SUAMEDIA

TAWA kuwachukulia hatua maafisa na askari wake watakao bainika kujihusisha na vitendo vya rushwa

 

Na.Vedasto George

Kaimu  Kamishna  Mkuu wa  Mamlaka ya Usimamizi Wanyama Pori Tawa  Mabula Nyanda  amesema mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua maafisa  na  askari wake watakao bainika kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa utekelezaji majukumu yao .


Picha ya pamoja Kati ya Kaimu Kamishna wa uhifadhi mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania Mabula Misungwi Nyanda na Baadhi ya Maafisa wa TAWA.

Mamlaka ya Usimamizi wa Nyama Pori Tanzania Tawa ndiyo yenye jukumu la kulinda na kusimamia mapori yote ya akiba yaliyotengwa kisheria kwaajili ya uhifadhi.

Kutokana na umuhimu huo, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Mabula Nyanda  amekutana na askari kutoka kanda zote za uhifadhi nakutoa onyo kwa maafisa hao ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria zilizowekwa na Taifa.


Baadhi ya Maafisa wa TAWA waliohudhuria katika kikao kazi Cha kujadili Mambo mbalimbali ya Mamlaka hiyo wakimsikiliza Kaimu Kamishna wa uhifadhi mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania Mabula Misungwi Nyanda.

“Hatutamvumilia mkuu yeyote wa kituo ambaye atakuwa anaona vitendo vya rushwa kwa baadhi ya askari wa tawa na hachukui hatua badala yake tutaanza kwa kumshughulikia yeye halafu askari wengine watafuata” Kamishna Mabula alisisitiza.

 Akizungumzia Kuhusu mikakati ya kukabiliana na wanyama wasumbufu kwa binadamu na mali zao,kamishna Nyanda  ameeleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo.


Kaimu Kamishna wa uhifadhi mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania Mabula Misungwi Nyanda, akizungumza na Maafisa wa TAWA waliofika katika kikao kazi Cha kujadili Mambo mbalimbali ya Mamlaka hiyo leo Mjini

“Katika mikakati ya Tawa, tumejipanga kuhakikisha tunalinda mapori yetu yote ili kuepuka matukio ya ugaidi kufanyika kisha magaidi hao kukimbilia kwenye maeneo hayo na kuyafanya kuwa maficho na kuyageuza kuwa viwanja vya mafunzo” .Kamishna Mabula aliongeza. 

 


Kwa upande wao baadhi ya Maafisa wa TAWA waliohudhuria kakao hicho wamesema madhara ambayo amekuwa yakijitokeza kwa wananchi kuvamiwa na kuuawa na wanyama ni kutokana na uelewa mdogo wa wananchi hivyo wao kama watendaji watahakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi hao.

 

 



 




Post a Comment

0 Comments