SUAMEDIA

SUA yatoa mafunzo kwa watafiti vijana.

Na. Ayoub Mwigune.

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimeandaa mafunzo ya siku mbili ya wafanyakazi kwa wanataaluma na waendeshaji ili kufanya tafiti bunifu ambazo zinalengo la kutoa suluhisho la changamoto zinazoikabili jamii.


Akifungua mafunzo hayo katika katika Kampasi Edward Moringe zamani ikijulikana kama Kampasi Kuu Makamu Mkuu wa hicho ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo Prof. Chibunda amesema SUA imeandaa mafunzo kwa ajili ya watafiti vijana ili kwenda kufanya tafiti ambazo zitazaa matunda katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi. Kwa upande wake Prof. Samwel Kabote ambaye amemwakilisha Naibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Maulid Mwatawala amesema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa sana kwa washiriki ili kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti . Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kurugenzi ,Uzamili, Utafiti, Uhaulishaji wa Teknolojia na Ushauri wa Kitaalam SUA Prof. Esron Karimuribo amesema mafunzo hayo ni kwa ajili kufahamu kwa upana namna ya kufanya tafiti Mafunzo hayo yatawasaidia kuwajenga uwezo wa kujua namna ambavyo wanaweza kuifadisha jamii kutokana na tafiti zao pamoja na kutambua changamoto mbalimbali zinazo ikakumba jamii lakini pia namna ya kuweza kuuza mawazo.

xxxxxxxxxx


Post a Comment

0 Comments