Na.Vedasto George
Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyama Pori Tawa
Mabula Nyanda amesema mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua
maafisa na askari wake watakao bainika kujihusisha na vitendo vya
rushwa wakati wa utekelezaji majukumu yao .
Kutokana
na umuhimu huo, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Mabula Nyanda amekutana
na askari kutoka kanda zote za uhifadhi nakutoa onyo kwa maafisa hao ili
kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria zilizowekwa na
Taifa.
“Hatutamvumilia mkuu
yeyote wa kituo ambaye atakuwa anaona vitendo vya rushwa kwa baadhi ya askari
wa tawa na hachukui hatua badala yake tutaanza kwa kumshughulikia yeye halafu
askari wengine watafuata” Kamishna Mabula alisisitiza.
Akizungumzia Kuhusu mikakati ya kukabiliana na wanyama wasumbufu kwa binadamu na mali zao,kamishna Nyanda ameeleza hatua zilizochukuliwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo.
Kaimu Kamishna wa uhifadhi mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania Mabula Misungwi Nyanda, akizungumza na Maafisa wa TAWA waliofika katika kikao kazi Cha kujadili Mambo mbalimbali ya Mamlaka hiyo leo Mjini
“Katika
mikakati ya Tawa, tumejipanga kuhakikisha tunalinda mapori yetu yote ili kuepuka
matukio ya ugaidi kufanyika kisha magaidi hao kukimbilia kwenye maeneo hayo na
kuyafanya kuwa maficho na kuyageuza kuwa viwanja vya mafunzo” .Kamishna Mabula
aliongeza.
Kwa upande wao baadhi ya
Maafisa wa TAWA waliohudhuria kakao hicho wamesema madhara ambayo amekuwa
yakijitokeza kwa wananchi kuvamiwa na kuuawa na wanyama ni kutokana na uelewa mdogo
wa wananchi hivyo wao kama watendaji watahakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa
wananchi hao.
0 Comments