SUAMEDIA

SUA yafaidika miaka mitano ya JPM

 Na Gerald Lwomile

SUA - Morogoro

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA leo kimezindua kitabu kinachoeleza mafanikio ya Chuo hicho katika kipindi cha miaka mitano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambapo kimefanikiwa kujiimarisha katika miundombinu ya kufundisha na kufundishia ikiwemo madarasa, maabara, karakana pamoja na mashamba ya chuo.

 


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais , Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro wa tatu kulia na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo wa pili kulia wakizindua kitabu cha mafanikio ya miaka mitano ya SUA

Akizungumza leo Octoba 12, 2020 wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanywa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais , Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amesema awali chuo hicho kilikuwa kinakabiliwa na hali mbaya ya miundombinu lakini Serikali ya awamu ya tano imefanya juhudi katika kuhakikisha SUA inasonga mbele

Amesema kutoka na changamoto hizo hata idadi ya wanafunzi ilianza kupungua chuoni hapo jambo ambalo lilihatarisha chuo kushuka katika ubora ambao hata hivyo hivi sasa umepanda

“Kama nilivyosema mwanzo chuo chetu kilikuwa kinakabiliwa na changamoto nyingi mno lakini changamoto kubwa ilikuwa kwenye miundombinu ya kufudisha na kufundishia hasa madarasa, maabara, karakana pamoja na mashamba ya chuo kwa kweli yalikuwa yamechakaa kwa kiwango ambacho yalikuwa yanatatiza ufundishaji”amesema Prof. Chibunda

Prof. Chibunda amesema hata miundombinu mingine kama barabara ilikuwa pia hairidhishi ambapo barabara nyingi zilikuwa zimechakaa na katika kipindi cha masika kuna baadhi ya maeneo ya chuo yalikuwa hayapitiki na pia viwanja vya michezo navyo vimeboresha

Akizungumzia mashamba ya mfano yaliyoanzishwa chuoni hapo Chibunda amesema yamesaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo na hasa kutokana na maeneo mengi kuwa na wasiwasi wa wanafunzi kwenda wakihofia ugonjwa wa COVID 19 ambao hata hivyo kwa sasa haupo nchini

Amesema zaidi ya wanafunzi 2000 wamefanya mazoezi kwa vitendo na kuwa walionyesha ustadi mkubwa tofauti na miaka ya nyuma ambapo waliona kushiriki katika shughuli za shamba pengine si jambo zuri

“Mwaka huu hapa chuoni kwetu wanafunzi zaidi ya 2000 wamebaki hapa chuoni kwetu na kujigunza kwa vitendo, nipende kusema kuwa tumepata mafanikio mengine makubwa kwa sababu kwa kweli miaka ya nyuma wanafunzi wengi walikuwa wanakuwa wagumu kushiriki shughuli za shamba kwa mikono yao lakini mwaka huu wamefanya maajabu wameshiriki katika nyanja zote” amesema Prof. Chibunda

Makamu Wakuu wa Vyuo na Manaibu Makamu Wakuu wa vyuo wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa kitabu hicho
 


Prof. Chibunda katikati akizungumzia mafanikio ya miaka mitano ya chuo hicho katika awamu ya tano, kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais , Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro
KATIKA VIDEO


Post a Comment

0 Comments