Na: Vedasto George
Mkuu
wa mkoa wa Morogoro LOATA OLESANARE
amewataka wanachi wote waliojiandikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura katika mkoa huo kuakikisha
wanatimiza haki yao ya kikatiba
ya kuchagua viongozi
watakao weza kuwatumikia kikamilifu na kusimamia rasilimali za nchi.
Olesanare
ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi
ya Uchaguzi mkuu wa wa Rais, Wabunge na Madiwani utakao fanyika tarehe 28 mwaka
2020 na kusema kuwa mkoa wa Morogoro unajumla ya ya vituo vya kupigia kura Elfu nne na miasaba
na sabini na nne (4,774) huku wapiga
kura ambao walijiandikisha wakiwa ni zaidi ya
milioni moja (1,623,629).
Aidha
Sanare amesema kuwa maandalizi ya kuakikisha wananchi wanatimiza wajibu wao
tayali umekamilika ambapo vifaa vya uchaguzi tayali vimekwisha pelekwa
majimboni huku akisisitiza kuwa vituo vyote vya kupigia kura vitafungulia
saamoja asubuhi kama ilivyo tangazwa na Tume ya taifa ya uchaguzi NEC.
INSERT..Wananchi ambao
watashiriki kupiga kura ninawasihi kurejea makwao mara tu baada ya kupiga kura ili kuendelea na shughuli zao
za kawaida huku wakifuatilia matokeo ya
uchaguzi kupitia runinga na vyombo vingine vya habari.Pia wananchi wote nawasihi kujiepusha kushiriki kwenye makundi
yoyote yenye viashiria vya kufanya vurugu au kuendelea kusimama kwa makundi
karibu na vituo vya kupigia kura”.Amesema mkuu huyo wa mkoa Loata Olesanare.
katika video
0 Comments