SUAMEDIA

SUA tena kushiriki Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Mashariki


Na: Gerald Lwomile

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kinaendelea na maandalizi
ya kushiriki maonesho ya wakulima nanenane Kanda ya Mashariki na
yale ya Kitaifa yatakayofanyika mkoani Simiyu kuanzia tarehe 1 hadi
8 Agosti 2020

Akizungumza katika kikao cha maandalizi ya maonesho hayo
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Kujiendeleza ICE chuoni hapo
Prof. Dismas Mwaseba amesema maandalizi ya maonesho hayo
yanaenda vizuri na wakulima wakubwa na wadogo watanufaika
wakifika banda la SUA
Naye Mratibu wa maonesho hayo kutoka Taasisi ya Elimu ya
Kujiendeleza Dkt. Innocent Babili amesema tayari menejimenti ya
SUA ikiongozwa na Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael
Chibunda imewataka waoneshaji kutoka chuoni hapo kupeleka
teknolojia na ubunifu unaoweza kuwasaidia wakulima
Amesema katika maonesho ya wakulima nanenane wakulima na
wananchi kwa ujumla watarajie kujionea teknolojia na ubunifu mpya
ambao kama watauchukua na kuufanyia kazi unaweza kuinua kwa
kiasi kikubwa maendeleo yao

Maonesho ya Wakulima nanenane mwaka 2020 yamebebwa na
kauli mbiu isemayo” Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
chagua viongozi bora”









Post a Comment

0 Comments