Vedasto George.
Licha ya Rais wa Jamhuri ya Muungamo wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kukumea na kudhibiti wabazilifu wa fedha za umma sambamba na watendaji hewa, Hali hii inaendela kujitokeza katika chama cha ushirika TURSACCOS mkoani Morogoro ambapo wanachama wamebaini upotevu wa fedha Zaidi ya shilingi bilioni moja na kuiomba serikali kuwasaidia ili wausika waweze kuchukuliwa hatua walio husika na wizi huo.
Hayo yamebainika katika mkutano mkuu wa 20 wa wanachama cha Akiba na mikopo TURSACCOS Mkoani Morogoro hambapo wanachama wamehoji hatua iliyofikiwa baada ya kuwabaini watu waliohusika na ubadhilifu wa fedha za chama, Zaidi ya shilingi bilioni moja 1 huku waliokuwa wakilipwa fedha hizo kutokuwa wanachama hai pia watumishi wa ushirika na baadhi ya fedha hizo zikiingizwa katika akauti za watu wengine ambao ni wanachama ikiwa ni kinyume cha sharia
Kwaupande wake Afisa Ushirika mkuu halmashauri ya wilaya ya mvomero Dausoni Kikalungaa amekili kuwepo kwa wizi wa fedha ndani ya ushirika huo na kuwataka wanachama kuwa wavumilivu wakati swala hilo likishughulikiwa na kusema baadhi ya watu ambao walihusika katika wizi huo wapo nje ya mkoa wa Morogoro na taratibu za kuwarejesha kujibu tuhuma zinafanyika kupitia jeshi la polisi,Huku makamu mwenyekiti wa chama cha akiba na mikopo TURSACCOS Salome Kihula akiwataka wanachama kuto ingiza siasa katika shughuli za chama.
0 Comments