SUAMEDIA

VIONGOZI WAMEASWA KUKATAA KUTUMIKIWA BALI KUSIKILIZA NA KUTATUA CHANGAMOTO


Na: Mwandishi wetu
Viongozi  wameaswa kukataa kutumikiwa na kuwaogopesha watumishi wao,
hivyo wameshauriwa kuwasikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za
watumishi na wateja wao pindi wanapoleta shida zao. 



Wito huo umetolewa na Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo  (Utawala na Fedha) Mstaafu, Prof. Yonike Ngaka wakati akipokea
zawadi ya Ngao ya Utumishi uliotukuka katika hafla fupi ya kumkaribisha
rasmi  ndani ya Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii iliyofanyika
tarehe 02 Oktoba 2019 katika viwanja vya Ndaki hiyo chuoni SUA.
Akitoa shukrani kwa  uongozi na watumishi wote  wa Ndaki ya Misitu,
Wanyamapori na Utalii , Prof. Ngaga amesema amefurahishwa na mapokezi
aliyoyapata, hivyo ameahidi kushirikiana vyema na Ndaki hiyo ili kuweza kuleta
tija na maendeleo husika.
Kwa upande wake   Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo (Taaluma)
Prof. Peter Gillah amempongeza Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na
Utalii, Prof.   John Kessy kwa utaratibu anaoufanya wa kutambua juhudi za
viongozi wanaotoka katika ndaki hiyo na ameshauri utaratibu huo uendelee
kwa sababu unaleta faraja na ushirikiano katika kazi za kimaendeleo chuoni
humo.
Na pia amempongeza Prof. Ngaga kwa uongozi mzuri katika  kipindi chote cha
uongozi wake akiwa kama Naibu Makamu wa Mkuu wa Chuo
(Utawala na Fedha) 2014-2018.
Kwa upande wa Prof. Kessy ametoa shukrani kwa wote walioshiriki katika
kubadhibhi zawadi hiyo na pia ameahidi kuendeleza utamaduni huo ili
kuongeza ushirikiano na maendeleo chuoni SUA.


                                                  

Post a Comment

0 Comments