Mara nyingi michango ya wanawake katika sekta muhimu kama Teknolojia na sayansi haionekani lakini historia inaonesha jinsi gani wanawake walivyotoa mchango mkubwa hasa katika karne ya mapinduzi ya viwanda.
Leo nimeona nikuletee hii listi ya wanawake waliotoa mchango mkubwa katika kufanya vumbuzi mbalimbali za kisayansi duniani.
1:Florence Parpart. Mwaka 1914 Florence Parpart alivumbua friji la kisasa linalotumia umeme ambapo uvumbuzi huo uliweka rekodi ya dunia baada ya kuvumbuliwa na mwanamke.
2:Marie Van Brittan. Anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa katika uvumbuzi wa kamera ya cctv mwaka 1969,,ambapo ugunduzi huu aliufanya baada ya kukithiri kwa uhalifu katika jiji la Newyork.
3: Stephanie Kwolek . Stephanie Kwolek atakumbukwa kwa uvumbuzi wake wa material iliyotumika kutengeneza bullet proof.
4:Hedy Lamarr’s . Ni mwafizikia aliyebobea katika maswala ya mawasiliano ambapo aligundua teknolojia ya wireless iliyo saidia kuanzishwa kwa wiFi na mfumo wa GPS.
5:Josephene Cochrane. Mwaka 1887 Josephene Cochrane alivumbua machine ya kuoshea vyombo au dish washer ambazo alikua akiziuza mahotelini mwaka mmoja baadae alifungua kiwanda chake.
6:Letitia Gee. Mwaka 1899 Letitia Geer Alivumbua bomba la sindano na kubadilisha historia ya sekta ya afya milele.
7: Dr Maria Telkes. Dr Maria Telkes mwaka 1947 alijenga nyumba ya kwanza duniani yenye mfumo wa umeme wa jua au solar energy.
8:Maria Beasely. Mwaka 1886 Maria Beasely alibuni maboya ya kuogelea au life jackets baada ya kukithiri vifo vya baharini , ni uvumbuzi uliopongezwa na watu wengi na kumfanya Maria Beasely kua mwanasayansi mwenye jina kubwa.
9:Dr Shirley Jackson Ni mwanafizikia aliebuni nyaya au fiber cable zinazotomika leo hii kwenye mitandao ya simu, pia uvumbuzi wake mwingine ulio mjengea jina ni pamoja na machine ya fax, mfumo wa kusubirisha mtu kwenye simu au call waiting.
10:Ada Lovelace. Unaweza usiamini lakini computer programmer wa kwanza kabisa duniani ni mwanamke ,Ada Lovelace alikua mtu wa kwanza kubuni program mbalimbali za computer.
0 Comments