Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA
kimefanya Mkutano wa 115 wa Baraza kuu la wafanyakazi Juni 20 na kujadili taarifa mbalimbali zinazohusu Chuo pamoja na
ustawi wake.
Awali akifungua mkutano huo wa Baraza
Kuu la Wafanyakazi SUA Mwenyekiti wa Baraza hilo Prof. Raphael Chibunda aliwataka wajumbe kuimba wimbo wa
mshikamano ambao unaoshiria umoja na mshikamano kwa wafanyakazi.
Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni
Makamu wa Mkuu wa Chuo SUA Prof.
Chibunda amewataka wajumbe kushiriki kikamilifu katika kuitisha vikao
kwenye mabaraza madogo na kuhakikisha wanawasilisha hoja walizoziibua kwenye
mabaraza hayo madogo na hatimaye
kuyaleta kwenye baraza kuu la wafanyakazi la chuo ili yaweze kujadiliwa na
kupatiwa majibu.
Aidha amesisitiza kuwa mabaraza ambayo
yamekuwa hayana utamaduni wa kukaa yatafutwa endapo yataendelea kutokuzingatia
suala la kukaa kwenye mabaraza hayo madogo ambayo kimsingi yapo kisheria,
Baraza la wafanyakazi hufanyika mara nne
kwa mwaka ambapo kupitia mkutano huo wafanyakazi huweza kujadili mambo
mbalimbali na hufanyika wiki moja kabla ya mkutano mkuu wa baraza kuu la Chuo
0 Comments