SUAMEDIA

SUA YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA USAFI MANISPAA YA MOROGORO


Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kimeadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kuunga mkono
jitihada za serikali za kutokomeza mifuko ya plastiki katika manispaa ya Morogoro kwa wafanyakazi wote
wa SUA kufanya usafi kwenye soko la Manzese na barabara kuu iendayo chuoni hapo.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo kwa naiaba ya Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Raphael
Chibunda, Naibu makamu mkuu wa chuo  taaluma Prof. Peter Gillar amesema zoezi hilo litakuwa endelevu
katika kuhakikisha manispaa ya Morogoro na maeneo ya chuo yanakuwa safi.
Naibu Makamu wa Mkuu wa chuo Taaluma Prof. Peter Gillah  kushoto akiwa pamoja na Naibu Makamu wa Mkuu wa chuo Utawala na Fedha Prof. Fredrick Kahimba katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.


Prof. Gillar amesema kutokana na muitikio mkubwa waliouonyesha wakazi wanaozunguka maeneo hayo
na wafanyabiashara ni imani ya chuo kwamba wananchi hao wataendelea kuunga mkono jitihada za SUA
na serikali katika kudumisha usafi katika manispaa ya Morogoro ambayo imekuwa na ndoto ya muda
mrefu kuwa jiji.
Naibu Makamu wa Mkuu wa chuo Taaluma Prof. Peter Gillah akizungumza na wafanyakazi wa SUA mara baada ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma 
Amesema hii sio mara ya kwanza kwa SUA kufanya usafi bali imekuwa ikifanya kila mwaka na sio kwenye wiki
tuu ya utumishi bali itaendelea kufanyika kwenye kila siku muhimu za kitaifa na kuomba mshikamano huu
uendelee ili kuwe na  dhamira ya pamoja ya kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na kuboresha afya za
wananchi kwa kuepuka magonjwa ya mlipuko kama kipindupindi kinachosababishwa na uchafu.
Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga na kutoa shukrani kwa wanajumuiya wa
SUA na wananchi kwa kufanya kazi hiyo Naibu makamu mkuu wa Chuo Utawala na Fedha Prof. Fredrick
Kahimba amewashukuru wanajumuiya wote wa SUA kwa kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hilo ambalo
limeleta msisimko wa aina yake kwa jamii.
Amesema kwa mujibu wa maelekeozo kutoka ofisiya rais manejiment ya utumishi wa Umma na utawala
bora ilitoa maelekezo kwa taasisi zote za umma kufanya mambo mawili katika maadhimisho ya wiki ya
utumishi wa umma kushiriki kwa kufanya shughuli za kijamii katika maeno  ya wananchi wanakopata
huduma au kukutana na watumishi katika maeneo yao ya kazi ili kusikiliza maoni na changamoto
wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao na wadau wan je kupata mrejesho wa huduma
wanazozitoa.
 Naibu Makamu wa Mkuu wa chuo Utawala na Fedha Prof. Fredrick Kahimbab  akishiriki kufanya usafi katika Eneo la Manzese sokoni  katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.
Naibu huyo makamu mkuu wa chuo Utawala na fedha amesema ana imani kuwa wananchi kwenye maeneo
yao pia waendelea kutokomeza mabaki ya mifuko ya plastiki iliyopo kwenye maeneo yao ili kuhakikisha mifuko
hiyo imekwisha kabisa katika manispaa ya Morogoro na Tanzania kwa ujumla kwa kuiga mfano huo.
Prof. Kahimba amewashukuru viongozi wa manispaa ya Morogoro ambao wametoa magari ya kukusanya
taka hizo na kwenda kuzitupa hali ambayo imerahishisha utekelezaji wa zoezi hilo na kuwaagiza viongozi wa
Idara ya Miliko na Uhandishi kuhakikisha taka zote zilizokusanywa katika zoezi hilo zinaondolewa na
kuteketezwa kabisa.
Nae Afisa tawala Mkuu wa SUA Peter Mwakiluma amewashukuru wafanyakazi wote kwa kujitokeza kwa
wingi na hiki ambacho SUA imekifanya itakiwasilisha sehmu husika katika Ofisi ya rais menejimenti ya utumishi
wa umma na utawala bora.
Amesema Chuo kilimua kufanya shughuli hii ambayo kufanya kazi kwenye eneo hilo la jamii kama taasisi kitu
ambacho kimeonekana kufanikiwa zaidi kutokana na muitikio wa wafanyakazi wenyewe na jamii katika kuweka
barabara ziwe safi na masoko ambayo wananchi wanayatumia kupata huduma mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments