SUAMEDIA

MICHEZO





TIMU ZA KIKAPU ZITOE HAMASA KWA WATOTO KUCHEZA MCHEZO HUO


Na Alfred Lukonge

Wito umetolewa kwa timu za mpira wa kikapu hapa nchini kuhamasisha watoto wadogo kujifunza mchezo huo hasa wale wa shule za msingi ili kukuza maendeleo ya mchezo huo kwa miaka ya baadae.

MOHAMED YUSUPH WA KWANZA KUSHOTO AKIWA NA WACHEZAJI WENZIE WA SAVIO

Wito huo umetolewa na mchezaji wa mchezo huo ambaye pia ni mkufunzi  kutoka timu ya Savio Mohamed Yusufu alipozungumza na SUAMEDIA.

 “nathamini sana maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu hapa nchini ndio maana nimeanzisha programu mahususi kwa watoto wadogo kila siku ya Jumamosi kuanzia saa mbili na nusu asubuhi mpaka saa sita na nusu mchana katika viwanja vya Don Bosco Upanga”.alisema Yusufu.

Pamoja na hayo Yusufu aliwataka waandishi wa habari za michezo hapa nchini kuacha kuupa kipaumbele mchezo wa soka pekee na kuangalia michezo mingine, jambo ambalo kwa upande wake anaona itakuwa ni njia mojawapo ya kukuza michezo mingine pamoja na kuiongezea mashabiki.

 Yusufu alianza kucheza mpira wa kikapu mwaka 1996 kipindi akiwa darasa la sita katika shule ya msingi Muhhimbili baada ya kuvutiwa na wachezaji nguli wa timu hiyo Peter Bategeki na Dorii Nima na ndoto zake ni kucheza mashindano ya dunia ya mpira wa kikapu.




YANGA KUKUBALI KICHAPO 3-1

Na: Fadhila Kizigo     

Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Tp Mazembe dhidi ya Yanga umemalizika kwa Yanga kukubali kipigo cha magoli 3-1 ikiwa ugenini DRC.



Mshambuliaji Bolingi wa Tp Mazembe aliifungia timu yake goli la kwanza kipindi cha kwanza dakika ya 28 na hadi kipindi cha kwanza kuisha Yanga bila kurudisha goli.

Kipindi cha pili katika dakika ya 11 Rainford Kalaba aliifungia Tp Mazembe goli la pili kabla ya kuifungia goli la tatu mnamo dakika ya 64.

Katika kipindi hichphichp cha pili cha mchezo Hamis Tambwe aliiandikia goli pekee la Yanga na hadi mchezo ulipomalizika TP Mazembe 3 na Yanga 1 na hivyo Tp Mazembe  imepata nafasi ya kuongoza kundi A kwa pointi 13 ikifuatiwa na Bejaia yenye pointi 8.





NDANDA KUMINYANA NA MWADUI YA SHINYANGA LEO





Ligi  Kuu  Tanzania  Bara  itaendelea  tena  leo Jumatano  Agosti 24, 2016  kwa kucheza mchezo mmoja, ambapo  Toto  Africans   ya  Mwanza itaikuwa   mwenyeji  wa  Mwadui FC.





Mwadui FC  inacheza  ugenini ikiwa  inarekodi  nzuri  ya  kushinda  michezo  mitatu  mfululizo ya  mwisho  katika  ligi  kuu  Tanzania  bara  wakati  Toto  Africans ikiwa imeshinda  mchezo  mmoja kati  ya mitatu  ya hivi  karibuni.


Mchezo  huo  utachezwa  katika  dimba  la  CCM  kirumba  majira  ya  saa 10:05  kwa  saa  za  Afrika  ya  mashariki.
                 
Timu  hizo  hazijacheza  mchezo  wowote  wa msimu  mpya  wa 2016-2017 wa ligi  kuu  Tanzania bara  ikiungana  na Yanga SC.


 

 

 

NDANDA YAJIFUA KUIVAA MTIBWA



Na:Adam Ramadhan

Klabu  ya  Ndanda  FC  imeweka  kambi  ya mazoezi  ya  siku  tano  mkoani  Morogoro   katika  uwanja  wa Chuo Kikuu  cha Sokoine  cha  Kilimo (SUA),  kwa  ajili  ya  kujifua  na kujiandaa  na  mchezo  dhidi  ya  Mtibwa  Sugar katika  mchezo wa pili  wa  Ligi  Kuu  Tanzania Bara.



Akizungumza  na  SUAMEDIA  Afisa  Habari  wa  Klabu  hiyo  Idris  Bandali  amesema   kuwa  kambi  hiyo  imeanza  jana  jumatatu  na  itamalizika  ijumaa  ya  wiki  hii, “Mazoezi  haya  yatakuwa  yanafanyika  asubuhi  tu  na   tunajipanga   ili   kufanya  vizuri   mara  baaada  ya  kupoteza  mchezo  wa kwanza  dhidi  ya  Simba, kwa  hiyo  mashabiki   wa  Ndanda  FC  watarajie  matokeo  mazuri  tu dhidi  ya  Mtibwa  Sugar”  alisema  Bandali.

Hata  hivyo  amesema  kuwa  lengo  lao kubwa  msimu  huu  ni  kumaliza  ligi ikiwa  katika  tatu  bora  na ikiwezekana  kuleta  upinzani  mkubwa  katika ligi hiyo, kwa  kupambana  vilivyo  ili  kufanya  ligi   iwe  ya  ushindani.

Ndanda  FC  ilipanda  daraja  msimu  wa  mwaka  2014/15  na  kumaliza  ligi  ikiwa  nafasi  ya tisa  msimu  wa 2015/16, tayari  msimu  huu imepoteza  mchezo  wake  wa  kwanza  dhidi  ya  Simba, na  hivyo  jumamosi  itacheza  na  Mtbwa Sugar kwa jihadi  ilikuata   matokeo  mazuri.

 

 

  

YANGA KUIVAA MAZEMBE LEO

 

Na:Adam Ramadhan

Klabu  ya  Yanga  leo itakuwa  mgeni wa  TP Mazembe  Mjini  Lubumbashi  Congo DR  kucheza  mchezo  wao  wa  kukamilisha  ratiba  ya  kundi  A  katika  kombe  la  shirikisho  Afrika  mchezo  utakaochezwa majira ya  saa 9:30 kwa  saa   Afrika  ya  mashariki.




TP  Mazembe  wanaongoza   kundi  hilo   wakiwa  na  alama   10   wakifuatiwa  na  Medeama  wenye  alama  8,nafasi   ya  tatu  ikishikwa  na  MO Bejaia  yenye  alama  5  huku  klabu   ya Yanga  ikiburuza  mkia  kwa  alama  4.

Kuelekea  mchezo   huo  Yanga SC  itawakosa  baadhi  ya wachezaji  kutokana  na majeraha   na  adhabu  ya  kadi  za  njano, Watakaoukosa  mchezo  huo kutokana na majeraha  ni  Obrey  Chirwa, Nadir  Haroub, Juma  Abdul  na  Vincent  Bossou  wakati  Donald  Ngoma  na   Kelvin  Yondani wataukosa mchezo  huo  kutokana  na  kadi mbili   za  njano.

Ushindi  au  sare  ya  aina  yoyote  itaivusha  Medeama  kwenda  nusu   fainali  huku  MO Bejaia  ikihitaji  angalau  goli mbili  iweze  kufuzu hatua  hiyo  ya nusu  fainali .

 

 

ELIMU YA SANAA IFUNDISHWE TOKA SHULE ZA AWALI: MWANIKE



Na: Alfred Lukonge

Imeelezwa kuwa  elimu ya sanaa ianze kufundishwa toka shule za awali kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kupelekea Taifa kuwa na hazina kubwa ya watu wenye vipaji  pamoja  na kutengeneza ajira binafsi.

MSANII HILIMALI AKIWA NA NGULI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA JUMA KASSIM NATURE



Hayo yamesemwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya Hilimali Mwanike Waukaya Jumatatu ya tarehe 21/8/2016 alipozungumza na SUAMEDIA na kubainisha kuwa “sanaa ni kazi kama kazi zingine hivyo serikali ikitia mkazo kwenye sanaa inaweza kuwa njia mojawapo ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wengi hapa nchini ”.
 
MSANII WA KIZAZI KIPYA HILIMALI MWANIKE AKIWA KATIKA STUDIO ZA SUAFM

Akizungumzia sanaa yake msanii Hilimali alibainisha kuwa hapo awali alikuwa dansa maarufu wa muziki wa bolingo alipokuwa mdogo na mara nyingi alijishindia zawadi mbalimbali kama Biskuti, Soda na Pipi zilizokuwa zinaandaliwa kama zawadi kabla ya kujitumbukiza rasmi katika muziki wa kizazi kipya.

Pia msanii Hilimali amemtaja mama yake mzazi Bi. Antonia Malundo maarufu kama mama  Maniponela ambaye alikuwa mcheza ngoma za asili maarufu miaka ya tisini katika wilaya ya Kilosa ndiye aliyemvutia kujiiingiza katika sanaa ya muziki, ndio maana hata muziki wake anaoufanya una vionjo fulani vya asili tofauti na wanamuziki wengine wa muziki wa kizazi kipya.

Pamoja na hayo Hilimali amebainisha kuwa vikwazo anavyokutana navyo kwenye ufanyaji wake wa kazi za muziki ni kukosa sapoti ya kutosha  kutoka kwa wadau wa muziki ambao mara nyingi wamekuwa   wakiweka mbele maslahi yao binafsi pasipo kumjali msanii.

Vilevile msanii huyo ametoa wito kwa serikali kuiwekea mkazo ahadi ya rais ya kulinda haki za wasanii kwani kwa mfumo ulivyo sasa hapa nchini inakuwa vigumu msanii kunufaika na jasho lake.

Msanii Hilimali alianza muziki akiwa darasa la nne mwaka  1995 alipokuwa anakaa na bibi yake wilaya ya Kilosa sasa hivi inatambulika kama wilaya ya Gairo kata ya Iyobo tarafa ya Chakwale kijiji cha Makuyu na matarajio yake ni kuwa msanii wa kimataifa.




MASHABIKI WA YANGA  WATOA MAONI KUHUSU MCHEZO WA YANGA NA AZAM FC

Na: Fadhila kizigo       

Mashabiki wa klabu ya Yanga wa mkoani Morogoro wametoa maoni yao kuhusu mchezo wa Ngao ya jamii dhidi ya Azam FC baada ya Yanga kufungwa kwa jumla mikwaju ya penati 4-1.
   

Akizungumza na SUAMEDIA Hassani Yanga amesema kuwa wachezaji wa Yanga imeonekana kulidhika na magori ya mapema hivyo kubweteka nakuruhusu upande wa wapinzani kuja juu hivyo kuwawia vigumu kumaliza vema katika dakika za lala salama.


 Ameongeza kuwa mchezo ulianza vizuri kwa kufanikiwa kufunga goli la kwanza kwa mkwaju wa penti ambapo gori lilifungwa na Donard Ngoma dakika ya 20 na kupata goli la pili dakika ya 21 ya mchezo.

Pia Bwana Hassani  ametoa wito kwa mashabiki wa Yanga kutokukata tamaa kwakuwa siku zote  matuta huwaga hayana mwenyewe kwaiyo yeyote anaweza kufunga na ndicho  kilichotokea tukakosa penati mbili na wapinzani kupata penati mbili.

Aidha Farid Mohammed alisema kuwa timu hiyo inahitaji mabeki wa kutosha na mechi nyingi za kimataifa kupata uzoefu katika kuimarisha timu na wapinzani wajipange kwa msimu unaoanza kwani kushindwa kwa mechi  dhidi ya Azam si kipimo kwao.   
 


            NEYMAR AIPA NGUVU TIMU YAKE KUFUZU MASHINDANO YA OLYMPIKI



Na:Adam Ramadhan

Mshambuliaji  wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Brazil  Neymar Junior ameisaidia timu yake ya taifa  kufuzu fainali katika  michuano  ya  Olimpiki inayoendelea kufanyika nchini Brazil.




Neymar  amefunga  goli la mapema  sekunde ya 14 na kuweka historia  ya kuwa goli la mapema zaidi katika michuano hiyo huku akifunga goli lingine dakika ya 90, Gabriel Jesus akafunga mara mbili,  Marquinhos na Luan pia na kukamilisha idadi ya magoli 6-0 dhidi ya Honduras.

Manchester City Gabriel Jesus akafunga mara mbili,  Marquinhos na Luan wakafunga pia kabla ya Neymar kuhitimisha mvua hiyo ya magoli kwa bao lake la dakika za lala salama kwa mkwaju wa penati.Brazil itakutana na timu kati ya Nigeria au Ujerumani kwa upande wa wanaume.

Wakati huohuo  Bingwa wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji kutoka Kenya Ezekiel Kemboi amenyang'anywa medali yake ya shaba aliyoishinda mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Hata hivyo Ufaransa ilikataa rufaa baada ya kubainika kuwa mwanariadha huyo  alikanyaga nje ya mstari wakati akishiriki mbio hizo Jumatano kuruka kiunzi na maji.




          YANGA YAPOTEZA MCHEZO NGAO YA HISANI DHIDI YA AZAM FC


Na:Adam Ramadhan



Mabingwa watetezi wa ligi  kuu  Tanzania bara klabu ya Yanga  imepoteza mchezo  wa ngao  ya  hisani  dhidi  ya  Azam FC kwa changamoto  ya mikwaju ya penati ,ukiwa ni mchezo wa ufunguzi  wa ligi kuu ya vodacom  inayotarajiwa kuanza  Jumamosi ya Agosti 20, 2016.







Mshambuliaji wa Yanga Mzimbabwe Donald Ngoma alifunga bao la kwanza dakika ya 20  ya kipindi cha kwanza kwa njia ya penati baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari na beki wa Azam David Mwantika.




David Mwintika anafanya tena makosa yanayosababisha Yanga kupata goli la pili kwa kushindwa kuumiliki mpira vizuri, ambapo Amisi Tambwe anachukua mpira na kumpasia Donald  Ngoma na kuweka mpira wavuni dakika ya 22.




 Dakika ya 74 ya kipindi cha pili  Shomari Kapombe aliipatia Azam bao la kwanza akitumia makosa ya mabeki wa Yanga walioshindwa kuondosha mpira kwenye eneo la hatari la goli lao.



Dakika ya 90 John Bocco anaisawazishia Azam FC goli la pili kupitia mkwaju wa penati baada ya beki wa Yanga kushika mpira ndani ya eneo la hatari,penati hiyo ambayo ilifanya matokeo kuwa 2-2 hali iliyopelekea kupigwa kwa mikwaju ya penati ambapo Yanga walipoteza mchezo huo.



Penati za Azam ziliwekwa wavuni na John Bocco,Himid Mao, Michael Balou na Shomari kapombe,huku penati ya Yanga ikifungwa na Deogratius Munishi pekee.
 

///////////////////////////////////////////////////////////////////////////////////
//////////////////////////////////////////////////////////////////////////////////

           

 KITENDAWILI NANI ZAIDI YANGA AU AZAM KUTEGULIWA LEO


 Na: Adam Ramadhani

Mchezo wa ngao ya jamii kati ya Yanga dhidi ya Azam utapigwa leo Jumatano Agosti 17,2016 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam majira ya saa 10:00 jioni ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara.


Kuelekea mchezo huo SUAMEDIA imezungumza na baadhi ya wadau wa soka mkoani Morogoro na kusema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwa timu zote kutokana usajili uliofanywa na vilabu hivyo.

“Mimi naipa nafasi Yanga kutokana na kiwango kizuri walichokionesha katika mchezo uliopita dhidi ya Mo bejaia” alisema Shukuru Omary  mkazi wa Mafiga. Naye Hussein Rajabu shabiki wa Simba amesema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na usajili wa klabu zote mbili.

Hata hivyo klabu ya Yanga itawakosa wachezaji wake watano akiwemo golikipa Ally Mustafa, mabeki Kelvin Yondani, Juma Abdul, Andrew Vincent na kiungo mshambuliaji Obrey Chirwa kutokana na matatizo mbalimbali yanayowakabili ikiwemo majeraha.

Mshambuliaji Donald Ngoma anatarajiwa kuwepo katika mchezo wa leo baada ya kukosekana katika mchezo uliopita wa shirikisho dhidi MO Bejaia kutokana na kadi mbili za njano alizopata katika michezo iliyopita.





RIADHA KUFUKA MOSHI LEO KATIKA VIWANJA VYA RIO DE JENEIRO

Na: Adam Ramadhani
 
Michezo ya Olimpiki kwa upande wa riadha itaendelea tena leo Agosti 17, 2016, Rio de Jeneiro nchini Brazil ambapo wanariadha kutoka nchini Kenya  na Uganda watayawakilisha  mataifa yao.


Timu ya taifa ya riadha ya Kenya itawakilishwa na wanariadha wake watatu Kipruto Conseslas, Ezekiel Kemboi na Brimin Kiprop  huku timu ya taifa ya Uganda ikiwakilishwa na Jacob Araptany katika mbio za mita 3000 za kuruka   vihunzi.

Lakini Kenya imeendelea kung’ara  katika michuano hiyo baada ya usiku wa jana mwanariadha Faith Kipyegon  kunyakua dhahabu ya tatu kupitia mbio za mita 1500 kwa wanawake, wakati kwa upande wa wanaume mjamaica Mc Leod alinyakuwa medali ya dhahabu kupitia mbio za mita 110.
 
 

                   CHELSEA YAIKUNG'UTA WESTHAM UNITED  2-1


                                                            
 Na: Adam Ramadhani

Mechi  za  mzunguko  wa kwanza wa ligi kuu ya England  zimekamilika usiku wa  Agosti 15 ,2016  mara baada ya Chelsea kuwafunga Westham United  magoli 2-1 katika dimba la Stamford bridge ,ikiwa chini ya kocha mpya Antonio Conte.

Chelsea walikuwa wakwanza kupata goli kupitia kwa Edern Hazard kwa  mkwaju wa penati dakika ya 47 mara baada ya Cesar Azplicueta kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari,Diego Costa aliipatia Chelsea goli la pili dakika ya 89,huku goli la Westham United likifungwa na James Collins dakika ya 77.



Kiungo mpya wa Chelsea Ngolo Kante aling’ara katika mchezo huo akishirikiana vyema kabisa na viungo wenzake kama Nemanja Matic, Edern Hazard na Emboaba Oscar,Chelsea wanaonekana kuleta ushindani katika ligi hiyo kutokana na soka safi la mashambulizi na kumiliki mpira  katika mchezo wa jana.

Ligi kuu nchini  England  itaendelea tena ijumaa ya wiki hii kwa mchezo mmoja kuchezwa  ambapo Manchester united watakapowakaribisha  Southampton majira ya saa 4:00 usiku katika uwanja wa Old Trafford.



     LIGI KUU YA ENGLAND YAENDELEA TENA LEO



Na: Adam Ramadhani
Ligi kuu ya nchini England itaendelea tena leo Jumatatu Agosti 15,2016,ambapo Chelsea  watawakaribisha Westham United katika dimba la Stamford Bridge majira ya saa 4:oo usiku.
 


Tayari michezo 9 imechezwa jumamosi na jumapili ya wiki iliyopita,mabingwa wa msimu uliopita Leicester city  wameanza vibaya  ligi hiyo mara baada ya kukubali kipigo cha magoli 2-1 kutoka kwa hully city,Crystal Palace walikubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Westbrom Albion huku  Swansea  1-0  wakiwafunga vijana wapya wa ligi hiyo Middlesbrough ,Manchester city ikiifunga Sunderland 2-1.


Klabu ya Southampton ilikubali sare ya 1-1 dhidi ya Watford, Tottenham ikibanwa mbavu ya suluhu ya 1-1 kwa Everton,huku Burney ikilizamisha sare ya goli 1-1 dhidi Stoke city,Manchester united inayonolewa na kocha mpya Jose Mourinho  iliibuka na ushindi wa jumla ya magoli 3-1 dhidi ya AFC Bournemouth.

Arsenal  ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Liverpool  kwa jumla ya goli 4-3 ,Arsenal  imekubali  kichapo cha magoli manne kwenye mchezo wa ligi kwa mara ya kwanza  tangu M\ay 2009 ilipochapwa na Chelsea jumla ya magoli 4-1.

Post a Comment

0 Comments