SUAMEDIA

Matokeo ya utafiti yaonesha Kilimo Biashara kina manufaa

Na: JOSEPHINE MALLANGO MASISI 

Matokeo ya utafiti wa Mradi wa Sera ya Kilimo Afrika (APRA), nchini Tanzania yameonyesha kuwa Kilimo Biashara kina manufaa kwa rika zote huku akina mama na vijana wanaonekana kunufaika zaidi  kwa kujipatia ajira kupitia mnyororo wa thamani katika kilimo hicho  .

Add caption



Hayo yamesemwa na  Prof. Aida Isinika wakati anaelezea matokeo ya utafiti wa Kilimo Biashara ulioanza nchini 2017-2021 katika semina ya waandishi wa habari iliyofanyika SUA mkoani Morogoro . 

Prof. Isinika amesema kilimo biashara ni mkombozi wa kutokomeza umasikini kwa wakulima kwa kuwa kinaboresha tija na ziada ambapo Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetakiwa kuongeza msukumo katika kutanua wigo wa mazao ya kibiashara ya muda mfupi nchini.

Prof. Isinika ambaye ni Mtafiti Kiongozi wa mradi wa (APRA) amesema mradi ulihusisha zao la Mpunga na Alizeti kwa kuwa ni mazao chanzo cha  chakula na uchumi na pia ni mazao ya muda mfupi  na  walichagua  wilayani Kilombero mkoani Morogoro na Ilamba na Mkalama mkoani Singida na kuwafikia Zaidi ya wakulima 500. 

Kwa upande wake Mtafiti wa mradi wa Sera za Kilimo Afrika (APRA )Prof. Ntegua Mdoe amesema matokeo ya utafiti wa mradi huo yanaonyesha manufaa kuanzia kwa wakulima wadogo wadogo  na jamii zinazozunguka maeneo hayo kwa kujihusisha na kilimo moja kwa moja au  katika mnyororo wa thamani 

Prof. Mdoe amesema wanaishauri  serikali kwa sasa iweke mkazo katika Kilimo Biashara kwa mazao ya muda mfupi  huku akisisitiza  uwepo wa mifugo katika maeneo ya kilimo kwa wakulima wa kati kwani imeonyesha kuwa na manufaa zaidi kwa matumizi  rahisi ya jembe la ng’ombe hasa kwa vijana na akina mama .

Nae Mtafiti Mwandamizi wa masuala ya Kilimo na Jinsia Dkt. Devotha Kilave  amesema katika utafiti huo waliangalia  mchango wa kilimo biashara katika kumsaidia mwanamke na kwamba uwepo wa uzalishaji mkubwa umeongeza mnyororo wa thamani ikiwepo viwanda  vya usindikaji na bidhaa zake zimekuwa zikimpa ajira mwanamke kwa kujialili  na kujipatia kipato cha uhakika na kupelekea kujiamini katika  kushiriki shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Washiriki Waandishi wa habari kutoka katika vyomba mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi
Mtafiti wa mradi wa utafiti wa sera ya kilimo afrika(APRA)Prof.Ntengue Mdoe akielezea kuhusu kilimo biashara na manufaa klwa jamii wakiwemo vijana

Post a Comment

0 Comments