SUAMEDIA

Rais wa Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa aishukuru Serikali ya Tanzania


Rais wa Afrika ya Kusini  Cyril Ramaphosa ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kushiriki katika harakati za ukombozi wa Afrika Kusini  kwa vitendo na kuahidi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo katika kuboresha miundombinu ,kubadilishana uzoefu na kukuza Teknolojia .
Rais wa Afrika ya Kusini  Cyril Ramaphosa akikipokea picha ya aliyekuwa mpigania uhuru Solomoni Mahlangu alipotembelea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.


Rais huyo amesema hayo wakati alipotembelea SUA na kuongeza kuwa anapoitazama
Mazimbu anaiona wazi  Afrika kusini ndani ya Tanzania na kwamba Tanzania ni nchi ya
kipekee ilivyoweza kuamasisha umoja na mshikamano kwa nchi za  afrika wakati wa
ukoloni na utawala wa kibaguzi.
Aidha ameongeza kuwa, Tanzania imeharimika kiuchumi kwa kuwa ililazimika kuharibu miundombinu yake hasa katika maeneo ya kusini ili kuzuia  watawala wa kibaguzi kuingia Tanzania na kuwavamia wapigania uhuru na ukombozi waliokuwepo wakimemo wa ANC kutoa afrika kusini. 
Rais wa Afrika ya Kusini  Cyril Ramaphosa akiwekashada la maua katika Mnara wa wapigania uhuru wa Afrika ya Kusini (ANC)
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema eneo la
Mazimbu lina uhusiano mkubwa na historia ya nchi hizo mbili kwani eneo hilo limebeba
historia muhimu ya kumbukumbu ya vuguvugu la ukombozi wa nchi Ya Afrika ya Kusini 

Nae Makamu wa Mkuu wa Chuo cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof . Rafael Chibunda
amemuelezea Rais Ramaphosa na ujumbe wake kutoka afrika kusini  historia ya chuo
cha na namna ambavyo Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere aliona
umuhimu wa kutoa majengo hayo ya wapigania uhuru  kwa chuo hicho kwa ajili ya
maendeleo ya kilimo nchini .
Rais Ramaphosa ametembelea katika maeneo mbalimbali ndani ya  Kampasi ya
Solomoni Mahlangu walipokuwa wakiishi wapigania uhuru, eneo la  makabuli ambapo
rais huyo ameweka shada la maua na kupanda mti ikiwa ni ishara ya muendelezo wa 
kumbukumbu ya uhusiano kwa vizazi vijavyo.


Post a Comment

0 Comments