Na: Siwema Malibiche.
Wanataaluma
nchini wametakiwa kutumia mawazo
yao vizuri kwa kuja na mikakati mipya itakayochochea maendeleo ya elimu kwa kukosoa, kushauri na kuboresha
ili kukuza sekta ya elimu
kwa maslahi ya Taifa.
|
Naibu Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo upande wa Mipango, Utawala na Fedha Prof. Amandus Muhairwa akifungua kikao |
Hayo yamebainishwa na Naibu Makamu Mkuu Mipango, Utawala na Fedha wa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Amandus Muhairwa wakati akifungua kikao cha wanataaluma
wa elimu ya juu kutoka vyuo mbalimbali nchini kilichofanywa kwa siku mbili
katika ukumbi wa ICE uliopo ndani
ya kampasi ya Edward Moringe Mkoani Morogoro.
Prof. Muhaimrwa amesema anatarajia wanataaluma hao
watajadili masuala mbalimbali ikiwemo maslahi ya wanataaluma,masuala ya viwango
vya elimu na maendeleo ya sekta ya elimu kwa upana wake ili kuboresha mazingira
ya kazi kwa wanataaluma hao.
Aidha, Prof. Muhairwa amefurahishwa na uamuzi
wa uongozi wa jumuiya ya wanataaluma wa elimu ya juu nchini kufanya kikao chao cha mwaka
katika Chuo Kikuu cha Sokoine Kilimo SUA huku
akiweka wazi kuwa anategemea kuwepo kwa mijadala mbalimbali itakayoleta tija katika maendeleo ya elimu kwa
kizazi kijacho kutokana na kuwepo kwa
wanatalauma bobezi na wazoefu.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Wajumuiya
ya Wanataaluma Tanzania (ASAPUCT) Dkt. Julius Edward Mtwenya amesema kuwa wamekutana SUA ili kufanya kikao
cha Baraza linalojumuisha Jumuiya ya Wenyeviti kutoka katika vyuo vikuu
mbalimbali nchini ikiwemo SUA na kutoa wito kwa wazazi nchini kuwekeza katika
kuwapatia elimu bora watoto huku
akiwataka makundi mbalimbali na wadau wa
elimu kutoa ushirikiano katika kuhakikisha maendeleo katika sekta ya elimu nchini.
Adha, amesema kuwa waanataaluma wanatakiwa
kuwekeza katika kufikiri ili kuleta mawazo mapya katika sekta ya elimu huku
akiipongeza Serikali, Mabaraza ya Wanataaluma
na wadau wa elimu kwa kuendelea kujipanga na kuona
jinsi gani wanaweza kutatua changamoto ili kukuza sekta hiyo ya elimu nchini.
Naye, Katibu wa Shirikisho la Jumuiya ya
Wanataaluma Tanzania Dkt. Maxmillian Chuchila amesema kuwa
mkutano huo utaleta mijadala yenye maslahi mapana itakayoleta tija kwa maendeleo ya elimu kwa kizazi kijacho na
kueleza kuwa amefurahi kuwa miongoni mwa washiriki katika kikao hicho na anaamini
maendeleo katika sekta ya elimu yatapatikana .
Kwa upande wake , Mhadhili kutoka Chuo kikuu cha
Ushirika Moshi ambae pia ni Katibu
kutoka Jumuiya ya Wataalamu Moshi Bi
Irene Biseko amesema kuwa kupitia mkutano huo kuna mambo mengi yataboresha vyuoni kwa kuzingatia ongezeko la idadi ya
wanafunzi wanao jiunga na elimu ya juu nchini na hasa kwa kuboresha mifumo na
kuishauri serikali.
0 Comments