Na:
Siwema Malibiche, Tatyana Celestine
Wananchi wametakiwa kuzingatia
upimaji wa udongo katika mashamba yao kabla ya kuanza kupanda mazao ili kutambua
ubora wa udongo, kilimo anachotakiwa kulima pamoja mbolea ya kutumia ili
kufanya uzalishaji wenye tija kwa maslahi binafsi na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Maabara kutoka Idara ya
Sayansi za Udongo na Jiolojia Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Bw.
Amour Mohamed amebainisha kuwa upimaji wa udongo unasaidia kutambua
ubora na afya ya udongo ambapo inampa uwezo mkulima kutumia maabara hiyo kutoa
majibu ya maeneo sahihi kulingana na
mazao husika.
Aidha amesema kuwa kupima udongo
kuna faida ya kumfanya mkulima kutambua Tindikali, Naitrojeni, Fosforasi, Potashiam,
Chumvi (EC) pamoja na aina ya udongo vitu ambavyo vinamsaidia kufanya uchaguzi
wa mbolea atakazotumia shambani na mazao gani anaweza kulima katika eneo hilo.
Mkuu huyo Maabara amesema wakulima wengi wamekosa elimu ya upimaji udongo kabla ya kuanza kilimo na kujihusisha na kilimo cha mazoea ambacho hakina faida kwao hivyo ni wakati kwao sasa kutambua elimu hiyo ya afya ya udongo na mimea ni muhimu pasi kusubiri kupeleka sampuli zao katika maabara baada ya kuona madhara.
Alipotakiwa kusema ni kitu gani
kingine wanapima mbali na udongo amesema kuwa kupitia Idara hiyo wanapima Mazao
na Samaki ili kutambua ubora wake kwa mlaji pamoja na kuangalia kiwango cha madini
Tembo (Heavy Metal) ambayo yanapatikana kwenye udongo au madawa yatumikayo
shambani kwani yakizidi hupelekea magonjwa kama kansa kwa mlaji.
Katika hatua nyingine Bw. Mohamed
amesema SUA imekuwa na kawaida ya kuwatembelea wakulima walipo pindi panapokuwa
na mradi ambao unalipa gharama zote lakini kwa sasa wanatakiwa kufika kufanya
vipimo na kupata ushauri wa kubadili mazao ili kuepuka hasara zinazopatikana
kwa kufanya kilimo cha mazoea .
0 Comments