Na Gerald Lwomile
Watumishi
wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) wametakiwa kuhakikisha wanaaminika
na kutegemeana katika utumishi wao ili kuleta tija na ufanisi kazini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuthibiti Uadilifu SUA Prof. Christopher Mahonge akifafanua jambo (Picha zote na Gerald Lwomile) |
Akizungumza na watumishi wa SUA Kampasi ya Mizengo Pinda iliyoko Wilayani Mlele Mkoani Katavi hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Kuthibiti Uadilifu SUA Prof. Christopher Mahonge amesema kuna baadhi ya watumishi wamekuwa na changamoto ya kukosa uaminifu na kushindwa kufikia malengo ya taasisi.
Amesema
mtumishi anapokuwa ni mwaminifu na tegemeo katika kazi yake inaisaidia Taasisi
kuwa na uhakika kuwa jakumu aliyopangiwa mtumishi yatatekelezwa kwa wakati na
kusaidia Taasisi kufikia malengo yake.
Prof.
Mahonge amesema watumishi wanapokuwa katika eneo moja mahusiano si yale mazuri pekee
kwani kuna wakati watumishi hutofautia lakini cha kujiuliza ni je mara baada ya
kutofautiana nini kinafanyika baadae ili kuhakikisha Taasisi inaenda kwa pamoja.
Awali
akimkaribisha Mwenyekiti wa KKU – SUA ili kuzungumza na wafanyakazi wa Kampasi
ya Mizengo Pinda, Naibu Rasi wa Kampasi ya Mizengo Pinda Mipango, Utawala na Fedha
Prof. Jeremiah Makindara amesema KKU inafanyakazi nzuri katika kuhakikisha
watumishi wanajua wajibu wao katika kazi.
Naibu Rasi wa Kampasi ya Mizengo Pinda Mipango, Utawala na Fedha Prof. Jeremiah Makindara akimkaribisha Mwenyekiti wa KKU kuzungumza na watumishi |
Amesema
ni wajibu wa watumishi kuzingatia uadilifu kazini na katika jamii kama inavyoelezwa
au kufafanuliwa na kamati hiyo kwani huo ndiyo mwongozo wa utumishi wa umma.
0 Comments