Na: Amina Hezron,Mbeya.
Serikali kupitia
Wizara ya Kilimo na Mifugo imenunua Pikipiki 61 kwaajili ya kuwapatia Maafisa
Ugani katika halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ili kuwasaidia kuwafikia walengwa
kwa haraka na kuwapatia ushauri wa kitaalamu utakaosaidia kuongeza uzalishaji wa
mazao katika halmashauri hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoni Mbeya Mwl. Missana Kwangura akimuanesha Mwandishi wa SUAMEDIA Amina Hezron Pikipiki hizo tayari kwa kugawawi kwa Maafisa Ugani.
Hayo yameelezwa na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoni Mbeya Mwl. Missana
Kwangura alipokuwa akizungumza na SUAMEDIA ofisini kwake na kuishukuru Serikali
ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwakuona changamoto wanazokumbana nazo
wataalamu wa Ugani ambapo na wao kama halmashauri wamenunua pikipiki nyingine
mbili kwa mapato ya ndani.
Ameeleza kuwa asilimia 85 ya mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali inategemea kutoka kwenye mapato ya ushuru wa mazao ambayo ni Mpunga au Mchele, Alizeti na Mahindi kidogo huku ikitegemea pia kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye upande wa mifugo hivyo pikipiki hizo zitasasaidia wakulima wengi kufikiwa na kuongeza uzalishaji hivyo halmashauri katika kufikia malengo yake katika ukusanyaji wa mapato.
“Wananchi watakapokuwa wanapewa ushauri wa
kitaalamu kuhusu mbinu bora za kilimo inamaa watazalisha zaidi kwa wafugaji pia
watapata ushauri kuhusu ufugaji bora na kupunguza magonjwa ya mifugo yao maana
yake watakuwa wanawapa ushauri na kuwafikia pamoja na kutibu kwa haraka na
kuongeza mali” alisema Mwl. Kwangura.
Aidha ameongeza kuwa pikipiki hizo zitakuwa na manufaa makubwa ya kuwarahisishia usafiri wa ndani ya kata na vijiji vyao lakini pia kufika makao makuu ya wilaya kwaajili ya vikao ambavyo hufanyika kila baada ya miezi mitatu ili kupeana mrejesho wa mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoni Mbeya Mwl. Missana Kwangura akizungumza na Mwandishi wa SUAMEDIA Amina Hezron kuhusu pikipiki hizo ofisini kwake. |
“Pikipiki hizi ambazo zimetolewa na Wizara tunashukuru kuwa zimeshafika tulimuita mtaalamu kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TAMESA) kutoka mkoani Mbeya tayari ameshazikagua na kuziona zipo sawa hivyo tunafanya utaratibu wa kukamilisha kuweka namba za usajili ili tuweze kuwagawia wahusika kama ilivyokusudiwa”,alisema Mwl. Kwangura.
0 Comments