Na: Amina
Hezron – Zanzibar.
Matokeo
ya utafiti yaliyofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Mradi
wa Chakula, Kilimo na Lishe (FoodLAND) yameonesha kuwa matumizi ya Matandazo ya
viwandani katika kilimo cha Maharage yameonekana kufanya vizuri ukilinganisha
na matandazo ya asili ambapo uzalishaji wake umeonekana kuwa mkubwa na yamesaidia
kwa kiasi kikubwa kupunguza uotaji wa magugu shabani.
Dkt. Boniface Massawe amabye ni mtafiti kutoka SUA kwenye Mradi wa FoodLAND akiongea na Mwandishi wetu Visiwani Zanzibar kuhusu utafiti huo wa matumizi ya Matandazo. |
Hayo yameelezwa
na Mtafiti kutoka SUA Dkt. Boniface Massawe alipokuwa akizungumza na SUAMEDIA wakati
wa Mkutano Mkuu wa tatu wa Mwaka wa Mradi wa Chakula Kilimo na Lishe (FoodLAND)
uliofanyika Visiwani Zanzibar na kusema kuwa katika utafiti huo yalitumika
matandazo ya asili, matandazo ya viwandani na sehemu nyingine hayakutumika
kabisa.
“ Wakati
tunafanya uangalizi baada ya uotaji tukagundua kwamba lile eneo ambalo lina
matandazo ya viwandani halikuwa na nyasi nyingi magugu hayakuota kwa wingi lakini
lile eneo ambalo halikuwa na matandazo kabisa lilikuwa na magugu kwa wingi sana
huku pale tulipoweka matandazo ya nyasi na mikunde kunde napo magugu yaliota
kidogo lakini siyo kwa kulinganisha na lile eneo ambalo halikuwa na matandazo
kabisa”, alisema Dkt. Massawe.
Dkt Massawe
ameeleza kuwa japokuwa uotaji wa mimea ya maharage katika sehemu isiyokuwa na
matandazo kabisa ulikuwa mkubwa lakini hayakuweza kufikia uzalishaji ambao
ulipatikana katika sehemu ambazo zilikuwa na matandazo.
“Hivyo
tumejifunza kwamba uotaji unaweza ukawepo lakini uzalishaji usiwe mzuri kama tulivyoona kuwa pamoja na huku kwenye
matandazo haya ya viwandani uotaji ulikuwa hafifu lakini bado uzalishaji
ulikuwa mkubwa ukilinganisha na uzalishaji katika haya matandazo mengine ambayo
ni ya asili na lile eneo ambalo halikuwa na matandazo kabisa “, alisema Dkt
Massawe.
Hivyo Dkt.
Massawe amewashauri wakulima kujitahidi kutumia matandazo ili kuongeza
uzalishaji kwakuwa hata katika jaribio hilo lilionesha kuwa uzalishaji wa
maharage ulikuwa mkubwa zaidi katika
eneo ambalo lilikuwa na matandazo ya viwandani ikifuatiwa na eneo lenye
matandazo ya mikunde kunde na nyasi .
Mkuu wa Mradi huo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Suzan Nchimbi Msolla akizungumza na Mwandishi wetu hii karibuni nje ya mkutano huo. |
Naye Mkuu
wa Mradi huo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Suzan Nchimbi
Msolla ameeleza kuwa njia hiyo ya kutumia matandazo inasaidia kuhifadhi unyevu
shambani lakini pia kwa kutumia aina hiyo ya matandazo aina ya kama plastiki
kutoka viwandani itawasaidia wakulima kuondokana na matumizi ya matandazo ya
plastiki ambayo hayaozi.
“Sisi tumejaribu na aina hiyo ya tandazo ambalo unaweza ukaliweka shambani na baada ya muda mara tu baada ya kuvuna mazao yako linaoza kabisa na kuchanganyika na udongo na linakuwa halina madhara kwa udongo”, alisema Prof. Msolla.
0 Comments