Adam Maruma - SUA
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), imeishukuru nchi ya Korea Kusini kupitia Shirika lake la KOICA, kwa ufadhili wa mradi wa vifaa venye uwezo wa kutunza wadudu kwenye ubaridi ambapo vifaa hivyo vinatarajiwa kutatua changamoto ya uhaba wa vifaa hivyo chuoni hapo kwa wanafunzi na watafiti.
Akizungumza wakati wa
makabidhiano ya vifaa hivyo Mkuu wa Idara ya Microbiolojia, Parasitolojia na Bioteknolojia
Dkt. Augustino Alfred Chengula amesema kwa awamu ya kwanza tayari chuo kimepokea
hadubini 3 na wanataraji kupokea vifaa vingine katika siku zijazo.
‘’Tuna kila
sababu ya kuwashukuru wenzetu hawa, kwa sababu wametuletea hadubini na pia
watatuleta friza, na kamputa moja ambayo itakuwa msaada mkubwa sana kwa ajili
ya kujifunzia wanafunzi wetu lakini pia kwa ajili ya kufanyia tafiti mbalimbali
zinazohusisha wadudu wanaoathiri wanyama
na binadamu’’ anasema Dkt. Chengula.
Mkuu huyo wa Idara ameongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia wanafunzi wengi kujifunza kwa wakati mmoja kwa kuwa sasa chuo kinapokea idadi kubwa ya wanafunzi na pia walimu wanaofanya tafiti zao vifaa hivyo vitawasaidia sana kufanya tafiti kwa urahisi zaidi.
Kwa upande wake kiongozi wa mradi
huo wa kuhifadhi wadudu ambae pia ni Mhadhiri
chuoni hapo Dkt. Jahashi Nzalawahe amesema mradi huo unalenga kuboresha
uhifadhi wa wadudu na utakua na awamu 4 na awamu ya kwanza itakua ni
ukarabati maabara ambazo zitatumika
kufundishia wanafunzi haswa wanafunzi wa shahada ya Umahiri na Uzamivu ambapo maabara 3 tayari zimekarabatiwa.
Dr. Nzalawahe amesema awamu ya
pili ya mradi huo, ambayo inaendelea sasa ni kuanza kuziboresha maabara hizo
kwa kuzipatia vifaa vitavyotumika katika kuwatambua wadudu hao pamoja na
kuwahifadhi kwa muda mrefu kwa kuwa friza zitakazoletwa zitakuwa na uwezo
mkubwa kwa kazi hiyo.
‘’Kilichofanyika
leo ni wenzetu kutoka Korea ambao ndio wadau wetu katika mradi huu wamekuja
kutukabidhi awamu ya kwanza ya vifaa ambavyo ni hadubini 3 ambapo hadubini 2
zitakuwa ma camera za kupiga picha na
kuzitunza kwenye computa na wanafunzi wataweza kuona kupitia computa hizo, na
sio lazima kupitia kwenye hadubini zenyewe’’ amesema Dk. Nzalawahe
Mtafiti huyo kiongozi wa mradi
amesema awamu ya tatu ya mradi kuwa
itajumuisha kuagiza vifaa ambavyo vitatumika katika ukusanyaji wa wadudu hao wa
wanyama mbalimbali wafugwao na wanyama wa porini.
Amesema awamu ya nne ya mradi
itakuwa ni kuagiza vifaa ambavyo vitatumika kufanyia ukusanyaji wa wadudu wa
Wanyama mbalimbali wafugwao na waporini na awamu ya 4 ya mradi itakua ni wadudu
hao kuhifadhiwa kwenye vifaa ambavyo vitaletwa kwa ajili ya kuhifadhia wadudu
hao, anasema Dk. Nzalawahe
Nae Dkt. Hansol Park ambae
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika hilo kutoka
Korea amesema mradi huo ulianza mwaka 2021, na wameamua kuanzisha Benki hiyo ya
wadudu SUA kwa ajili ya kusaidia kukusanya, kutafiti wadudu na kufugwa katika
maabara hizo ili kusaidia wanafunzi na watafiti.
0 Comments