Na. Vedasto George
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Mhe. Pauline Gekul amesema serikali kupitia Programu ya Urithi wa
Ukombozi wa Bara la Afrika itaendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine
cha Kilimo (SUA) kuyaendeleza, kukarabati na kutunza kumbukumbu zote za
kihisitoria zilizoachwa na wapigania
uhuru wa Afrika ya Kusini katika eneo la Kampasi ya Solomon Mahlangu.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul (kushoto) akiwasili katika Kampasi ya Solomon Mahlangu, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando na kulia Kaimu Rasi wa Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi Dkt. Geoffrey Karugila (Picha zote na Gerald Lwomile)
Mhe. Gekul ameyasema Januari 18,
2022 mjini Morogoro wakati alipotembelea
makaburi 97 ya wapigania uhuru wa chama cha ANC cha Afrika ya Kusini yaliyoko
Kampasi ya Solomon
Mahlangu na yanatunzwa na SUA kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni,
Sanaa na Michezo ambapo amesema mali kale na kumbukumbu zote za kihisitoria
zinapaswa kutunzwa vizuri ili vizazi vya
sasa na baadae viweze kutambua historia za nchi zao.
“Tutayatangaza tukishirikiana na Wizara ya Maliasili
na Utalii yawe ni maeneo ya vivutio ya
kiutalii wa kihistoria kwa wenzetu ambao wanapenda kupata historia
za nchi zao, lakini pia na watalii
wengine wafike kwenye maeneo haya kwa hiyo
tuko hapa kwa ajili ya kazi hiyo na
lengo ni kushirikiana na hizo nchi kwa
ukaribu ili tuone na wao wanashirikije katika kutunza historia hii” amesema Gekul
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul akisikiliza maelezo kutoka kwa Bw. Ali Mkopi mtumishi wa SUA anayelijua vizuri eneo hilo la Makaburi ya Wapigania Uhuru wa ANC
Aidha ameongeza kuwa kwa sasa Wizara
kwa kushirikiana na SUA kupitia Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la
Afrika inapaswa kutambua watoto na mama wa familia za wapigania uhuru wa Afrika
ya Kusini ili nao wawe sehemu ya historia pale zinapokuja familia zao kutoka
Nchi ya Afrika ya Kusini.
Mratibu wa Kituo cha Urithi wa
Ukombozi wa Bara la Afrika, Bw. Boniface
Kadili amesema eneo la Mazimbu ni sehemu
moja wapo ya Ukombozi wa Bara la
Afrika na jitihada zilizopo kwa sasa kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa
na Michezo ni kulitangaza katika gazeti
la Serikali ili eneo hilo liweze kuwa
katika Ulithi wa Taifa.
“Eneo hili likishalindwa kisheria sio kwamba linakuwa ni miliki ya Maliasili au
Wizara yetu bado litaendelea kuwa
miliki ya SUA ila sisi tunachofanya ni
kutoa ushauri wa kitaalamu wa kuhifadhi
eneo ili muhimu. Amesema Boniface Kadili Mratibu wa Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika “ amesema Gekul
Aidha Mhe. Gekul ameagiza Afisa
Utamaduni Mkoa wa Morogoro na Afisa Utamaduni Manispaa ya Morogoro kuhakikisha
wanatambua maeneo yote ya kihistoria ya asili ndani ya maneo yao ili kumbukumbu hizo zitumike
kwenye historia ya Tanzania.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,
Albert Msando amesema katika wilaya ya Morogoro yapo maeneo mengi ya kihistoria ya asili ambayo yanapaswa kutunzwa lakini changamoto kubwa iliyopo kwa sasa ni ukosefu wa watu ambao wanaweza kutunza maeneo
hayo hasa yanayohusu Machifu waliofia
katika wilaya ya Morogoro.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando (aliyevaa suti)
Akitoa taarifa ya namna ambayo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kilivyopewa majengo na maeneo hayo ya Kampasi ya Solomon Mahlangu kutoka kwa wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini Kaimu Rasi wa Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi, Dkt. Geoffrey Karugila amesema kambi hiyo ilianzishwa mwaka 1978 lengo likiwa ni kupigania uhuru wa Nchi ya Afrika ya kusini kupitia Chama cha ANC.
Dkt. Geoffrey Karugila ameendelea na kusema mwaka 1999 Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikabidhi eneo hilo rasmi kwa SUA ambapo mwezi Machi mwaka 1999 Baraza la Chuo
liliamua kubadilisha jina kutoka SUMAFUCO na kuliita Kampasi ya Solomon
Mahlangu na lina miundombinu mbalimbali iliyoachwa ikiwemo Madarasa, Hospitali na Jengo la Utawala.
0 Comments