SUAMEDIA

Wanajumuiya wa SUA wachangia Uniti 50 za damu ili kuokoa maisha.

 

Na : Gojo Mohamed.          

Uniti takribani 50 za damu zimefanikiwa kukusanywa kutoka kwa  Wanafunzi  pamoja na wanajumuiya wa  Chuo Kikuu cha  Sokoine cha Kilimo (SUA) katika zoezi la uchangiaji wa damu zitakazoenda kuwasaidia wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Wanajumuiya ya SUA wakichangia damu katika bonanza hilo


Amesema hayo Afisa Mhamasishaji Uchangiaji wa Damu kutoka hospitali hiyo,Bw. Mabruk Mbaruku kuwa katika Zoezi  la uchangiaji damu lililoambatana na Bonanza la michezo mbalimbali kwa pamoja  yamefanyika katika Viwanja vya  Kampasi Kuu vya Edward Moringe Sokoine.

Bw. Mbaruku ameeleza kuwa zoezi la uchangiaji wa damu ni muhimu sana kwa sababu hakuna sehemu ambayo unaweza ukapata damu zaidi ya kwa binaadamu mwenzio kwahiyo ni lazima jamii ihamasike ili iweze kuchangia damu.

Kwa upande wake SUA Dkt Charles Lymo kutoka Idara ya Sayansi ya Wanyama Viumbe Maji na Nyanda za Malisho, amesema  kuwa   wanajamii  wanapaswa kujijengea tabia ya kuchangia damu  kwa sababu suala la  ukosefu wa damu ni la dharula ili kuhakikisha vituo vinavyotunza  damu vinakuwa na damu ya kutosha  kwa ajili ya kuokoa maisha yao na  ya watu wengine.

‘‘Suala la uchangiaji wa damu ni muhimu, tunasikia kunakuwa na takwimu za ajali, lakina Wamama wanajifungua na wanakosa damu na kupelekea kupoteza maisha yao kwa hiyo benki zetu za damu zinapokuwa na damu ya kutosha inapelekea kuokoa Maisha ya watu na vizuri kuwa na utaratibu wa  kuchangia damu kwa sababu inakuwekea akiba na wewe mwenyewe pindi upatapo changamoto ya upungufu wa damu’’. alisema Dkt. Lymo.

Nae, Fatma Ibrahimu ambaye ni Mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Wanyama amesema kuwa ameweza kujitokeza katika zoezi la uchangiaji wa damu kwa mara yake ya kwanza kutokana na umuhimu ambao ameuona ambapo kuna wagonjwa wengi wanahitaji damu na zinakuwa zinakosekana.

Pia,amesema kuwashauri wanafunzi wenzie kujitokeza katika kushiriki masuala ya kijamii ikiwemo hilo la uchangiaji wa damu.

MATUKIO KATIKA PICHA YA BONANZA HILO LILILOKWENDA SAMBAMBA NA ZOEZI LA UCHANGIAJI WA DAMU.









Post a Comment

0 Comments