SUAMEDIA

Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi HEET chanzo cha unafuu katika Kilimo bora kupitia Kampasi ya Mizengo Pinda (SUA) Katavi

 


Na: Tatyana Celestine, Katavi


Wakazi wa Kijiji cha Kibaoni Kata ya Kibaoni mkoani Katavi wamekiomba Chuo Kikuu Cha Sokoine cha Kilimo SUA kuwasaidia kupata Elimu ya Kilimo na mbegu mara baada ya Mradi wa HEET kuonesha  ongezeko la Wanafunzi na Wakufunzi katika Kampasi ya Mizengo Pinda iliyopo Katavi.


Wanakijiji cha Kibaoni mkoni Katavi wakitoa maoni yao juu ya kufikiwa na Mradi  wakati wa Tathmini ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya kiuchumi



Akizungumza na SUAMEDIA wakati wa kufanya tathmini ya kuona wakazi wanategemea nini mara baada ya Mradi huo kuwafikia, Mmiliki wa Mashamba na Makazi katika eneo hilo Bw. Silas Damalu amesema kuwa kwake anaona unafuu mkubwa utatokea kwao kutokana na wataalam wa Kilimo kuja kufanya kazi hapo kwani watafaidika kutokana na Elimu itakayotolewa kuhusu Kilimo tofauti na ilivyo sasa.


Bw. Damalu ameongeza kuwa wakulima wamekuwa wakipata mbegu kutoka Zambia lakini pia wanategemea Bwana Shamba mmoja ambaye hatoshelezi kwa wote, hivyo kuwepo Kwa Kampasi hiyo na Mradi vitasaidia nao kupata unafuu katika ushauri na Elimu kuhusu Kilimo kama upandaji wa mbegu, ufugaji wa nyuki na utaalam zaidi.


Nao  vijana katika Kijiji hicho wamesema kuwa fursa nyingi zitajitokeza hata kama hawatasoma basi watafanya kazi kipindi cha utekelezaji wa Mradi.


Wameongeza kuwa mara baada ya kuanzishwa kwa Chuo hicho shughuli za ujenzi na Biashara zimekuwa kwa kasi kutokana na muingiliano ulioanza kuonekana na zaidi utakuwa wakati Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi unapotekelezwa ndani na nje ya Kampasi.


Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi HEET umezinduliwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda  uliolenga kuboresha elimu na kunufaisha Vyuo 14, uzinduzi uliofanyika Septemba 13, 2022 Jijini Dar es Salaam ambapo Kampasi ya Mizengo Pinda (SUA) Katavi imetengewa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani Milioni nane.








Post a Comment

0 Comments