Na.Vedasto George.
Wakulima wanaojishughulisha na Kilimo cha Mbogamboga na Matunda wa Kata ya Kiloka, Wilaya ya Morogoro wameiomba Serikali kuwafanyia Utafiti wa Udongo kwenye maeneo yao ya kilimo ili waweze kuzalisha mazao yenye ubora yanayoweza kushindana kwenye Soko la kimataifa.
Wakizungumza na SUAMEDIA wakulima Joseph John, Alima Kasimu na Shirima Amani wamesema kutokana na adha hiyo wanalazimika kutumia viuwatilifu mbalimbali vya kukuzia licha ya kutumia mbegu bora zenye uhakika wakutoa mazao ya kutosha.
Aidha wamesema licha ya kuzalisha mazao mengi lakini
changamoto kubwa ambayo inaendelea kutishia mazao yao ni uhaba wa soko ambapo kwa sasa wanalazimika kusafiri umbali
wa kilomita 25 kutoka kiroka mpaka Morogoro mjini lilipo soko la
mazao ya mbogamboga na matunda.
Katika kukabiliana na changamoto
hiyo Wadau wa Kilimo nchini wanaendelea kuonyesha jitihada za kuwasaidia
wakulima kwa kuwapa mbegu bora
za mazao ambazo zinatoa mazao mengi
ikiwemo viuwatilifu ambavyo
vinasaidia kuongeza uzalishaji.
Ebenezer Joseph ambaye ni Afisa
Kilimo kutoka Kampuni ya Mbegu Tanzania SEED COM LTD
amesema kwa sasa wao kama kampuni wameamua kujikita katika utoaji wa mbegu za mazao ya mbogamboga na matunda lengo likiwa ni kuwasaidia wakulima ambao wanafanya
kilimo hicho cha mboga na matunda.

0 Comments