Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, ameiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) kuwachukulia hatua mawakala wa mabasi wanaopandisha nauli kiholela, na kuagiza kuwa abiria wote waliozidishiwa nauli kurudishiwa.
Waitara ametoa maagizo hayo Desemba 21, 2021 alipofanya ziara katika kituo cha mabasi cha Magufuli kuangalia hali ya usafiri wa kwenda nje ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema kumekuwa na biashara mbovu ya tiketi na kupandisha nauli kiholela msimu wa sikukuu lakini pia ujanja ujanja wa kuandika nauli tofauti na aliyochajiwa abiria.
"Naelekeza wale wote waliozidishiwa nauli kurudishiwa kumekuwa na tabia abiria kuchajiwa nauli tofauti na iliyoandikwa kwenye tiketi
"Nimekagua kwenye magari nkakuta abira ametoa shilingi 60,000 lakini kwenye tiketi imeandikwa shilingi 40,000 au shilingi 35,000 huu ni wizi nimeagiza Latra kusimamia ili abiria warudishiwe nauli walizozidishiwa," ," amesema Waitara.
Aidha Waitara amesema suluhisho la abiria kulanguliwa ni kuanzisha mfumo wa tiketi mtandao ambapo ameahidi kuanza mwakani baada ya kukaa na wadau na kukubaliana.
0 Comments