Na.Vedasto George.
Mkoa wa Morogoro unakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa, vyoo, nyumba za walimu pamoja na madawati na kupelekewa kuwepo kwa msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule za msingi na Sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Olesanare katika Kikao cha Kamati ya Ushari ya Mkoa wa Morogoro (RCC) |
“Bila kuondoa upungufu wa miundombinu katika shule zetu watoto wetu watakosa haki yao yamsingi ya elimu bora nielekeze wakuu wa Wilaya na wakurugenzikatika halmashauri zote kusimamia miundombinu ya shule za msingi na sekondari” Alisema Loata Ole Sanare.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameleeza kuwa katika kipindi cha
miaka minne kuanzia mwaka 2016 hadi kufikia mwaka 2019 wanafunzi wapatao elfu
moja miamoja na tisini nanne 1,194 katika Mkoa wa Morogoro wamepata mimba za utotoni na kukatiza masomo yao.
“Mkoa kwa miaka mine idadi ya wanafunzo waliopata mimba ni1,194 tatizo ni kubwa na kwamaana hiyo nitoe wito kwa wenzetu wote na vyombo mbalimbali wachukue hatua za kisheria juu ya tatizo hili hali hii haikubaliki kwa namna yeyote ile nadani ya mkoa wa Morogoro, niwaelekeze Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kuakikisha wote wanaowapa watoto shule mimba kuakikisha wanachukuliwa hatua.” Alisema Loata Ole Sanare.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Morogoro Eng. Joyce Baravuga
amesema Mkoa tayari umeweka mikakati maalumu itakayowezesha kuimalisha ufaulu
ikiwemo kutumia mifumo ya TEHAMA katika ufundishaji, kuimalisha mifumo mbalimbali
ya ufundishaji na kujifunzia kwa wanafunzi pamoja na kuhamasisha wadau wa elimu kuendelea
kujitokeza kuchangia katika sekta hiyo
ya elimu.
Katika hatua nyingine
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa mwezi mmoja kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi kukamilisha
ujenzi wa vituo vya afya na Zahanati
katika maeneo yao na kusema kuwa kiasi cha shilingi bilioni 14 .7
zimetumika kufanya ukarabati wa
hospitali za zamani mbili na Zahanati
moja katika kipindi cha kuazia mwaka 2016
mpaka mwaka 2021.
Kikao cha Kamati ya Ushari ya Mkoa wa Morogoro
kimewajumuhisha wakuu wa wilaya zote za mkoa huo, wakurugenzi kamati ya ulinzi
na usalama mkoa, watumishi pamoja na wadau wengine wa maendeleo mkoani humo
lengo likiwani kujadili na kutathimini kazi za maendeleo zilizofanyika mkoani morogoro.
0 Comments