Na Vedasto George na Gerald Lwomile
Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA kupitia mradi wa “REFOREST” unaofadhiliwa na Serikali ya Sweden kwa kushirikiana na Shirika la maendeleo la SIDA kimeanzisha kozi mpya ya Shahada ya Uzamivu ya Sayansi za Misitu lengo likiwa ni kuzalisha wataalamu ambao watasaidia kutatua changamoto zilizopo kwenye misitu katika ukanda wa Afrika.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof. Raphael Chibunda (katika waliokaa) akiwa na viongozi mbalimbali wa Chuo na wanafunzi wa kozi ya Uzamivu waliosimama, kulia waliokaa ni Mratibu wa kozi Prof. Romanus Ishengoma
Akizungumza katika
mafunzo na wiki ya kuwakaribisha wanafunzi 20 kutoka nchi tano za Tanzania,
Rwanda, Uganda, Msumbiji na Ethiopia ambao wamechaguliwa kujiunga na kozi hiyo
mpya katika chuo cha SUA Prof. Romanus Ishengoma amesema ili kuwafanya
wanafunzi hao waweze kuwa mahiri katika masuala ya misitu watafanya tafiti mbalimbali
zinazojikita katika misitu ili kuona ni namna gani wanaweza kuja na majibu ya
changamoto zinazokabili misitu katika Afrika ikiwemo nchi zilizoko kusini mwa
Jangwa la Sahara.
”wanafunzi hawa Ili wote tuwalete kwenye uelewa unaofanana
tutawafundisha darasani kwa mwaka mzima, pili wanafunzi hawa watafanya utafiti kwenye nchi zao na kuandika
tafiti zile kwa kipindi cha miaka mitatu, wakiwa kwenye Nchi zao watasimamiwa
na walimu walioko kule kwenye kipindi cha masomo ya darasani hawatafundishwa na walimu walioko SUA tu tutachukua walimu pia kutoka kwenye vyuo vilivyo
kwenye nchi zao maana yake ni nini
tunachukua ukanda wa Afrika Mashariki na kidogo Kusini ili kutengeneza
progamu moja ambayo wote tunaunganisha nguvu”, amesema Pro.Romanusi
Ishengoma.
Akizungumzia matarajio
na faidi zitakazotokana na kozi hiyo Prof. Ishengoma amesema Chuo kitaweza kuzalisha wanafunzi ambao
wataweza kuondoa changamoto ya upotevu
wa misitu katika hichi hizo tano za Afrika na kusisitiza kuwa Chuo kitaweza kushirikiana na wadau ili kuweza kuzalisha
wataalamu ambao wataleta mchango mkubwa katika kuhifadhi misitu.
“Kupotea kwa misitu ni
tatizo kubwa na ili uweze kulitatua tatizo
hili kiutaalamu ni pamoja na kuwa na wataalamu wa kuweza kutatua haya kwahiyo sisi tutafundisha watu ambao watakuwa na upeo mkubwa wa kuweza kusaidia kutatua haya matatizo
makubwa ya misitu ambayo tunayaona misitu inapotea kila wakati, misitu
inabadilishwa matumizi kuwa ya kilimo kwenye kipindi ambacho tunategemea misitu
hii ichangie hasa katika suala zima la pato la Taifa” Amesema Prof.
Pro.Romanus Ishengoma.
Kwa upande wake Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha
Kilimo (SUA) Prof.Raphael Chibunda amesema
uwepo wa Mradi wa “REFOREST” SUA umedhihirisha ubora wa Chuo hicho Barani
Afrika na Duniani kwa ujumla
“Na uwepo wa huu mradi unaonesha ubora wa Chuo chetu ukilinganisha na
vyuo vingine katika ukanda huu wa Africa lakini na Duniani kwa sababu Chuo
chetu kilishindana na vyuo vikuu vya nchi
nyingine ili kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa program hii kwa sababu kuu ya
miundombinu ya ufundishaji katika maeneo
ya misitu ambayo chuo kimejiwekea kwa kipindi cha muda mrefu tukaweza kushinda
na kupewa nafasi hii” , amesema Prof. Chibunda.
Aidha Prof. Chibunda ameongeza kuwa SUA ndiyo Chuo Kikuu peke
yake katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambacho kinafundisha misitu na kuweza
kumiliki misitu ambayo inatumika kufundishia na kuweza kuzalisha mazao
mbalimbali yatokanayo na misitu.
“Sisi tuna eneo kubwa
la misitu katika mkoa wa Arusha pale Olomotonyi ambapo tuna zaidi ya hekta 800
za kupandwa lakini pia katika mkoa wa
Tanga kwenye milima ya usambaa eneo la Mazumbai tuna msitu wa asili karibu hekta
320, vilevile tumefungua shamba jipya la msitu lenye ukubwa wa hekta 10,000
msitu wa biashara katika mkoa wa Ruvuma” Amesema Prof Chibunda.
Zaidi ya Wanafunzi 300 kutoka mataifa mbalimbali waliomba
kusoma kozi hiyo ya Shahada ya Uzamivu ya
Sayansi za Misitu ambapo wanafunzi 20 tu ndiyo waliofuzu na kuwa na vigezo
huku watano wakiwa ni kutoka katika nchi ya
Tanzania, watatu kutoka nchini Msumbiji, wanne kutoka nchi ya Rwanda, wanne
kutoka Uganda, na wengine wanne ni
kutoka Ethiopia kati yao asilimia 45 wakiwa ni
wasichana.
0 Comments