Na: Tatyana Celestine
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Mradi wa Sekta ya Misitu (Wood cluster) kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kimefannya tafiti zinazoweza kusaidia ongezeko la uzalishaji wa mazao ya misitu kwa upande wa mbao ili kutokomeza uharibifu wa misitu nchini.
Akizungumza wakati wa kufungua warsha iliyolenga kusaidia
kupunguza upungu wa mahitaji ya mbao Tanzania leo 27/11/2020 Profesa Mshiriki
Idara ya Uchumi Misitu na Mazingira ambaye ni Mratatibu wa kitaifa wa mradi
Prof. Felista Mombo amebainisha kuwa Tanzania inaupungufu wa mbao unaokaribia
mita kyubiki milioni 19.5 ambao ni mkubwa ikilinganishwa na kiasi
kinachozalishwa nchini.
Kwa upande wake Kamishna Mhifadhi wa Program za Misitu
Tanzania Profesa Dos Santos Silayo amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeona
kuwa ni fursa nzuri kwa mradi huo kwani umeweza kukutanisha watafiti wa ndani
na nje ya nchi katika sekta ya misitu hivyo utafiti huo umeweza kuzalisha wataalamu
Zaidi wa utafiti ambao wamekuwa wakifanya tafiti katika maeneo ya masoko,
ukuzaji wa miti mashambani, ushirikishwaji wa jamii na kuonesha ushiriki wa
Tanzania katika soko la kimataifa.
0 Comments