SUAMEDIA

Umoja wa Mataifa wafanya mazungumzo na viongozi wa kijeshi katika mzozo wa Libya

 Viongozi wa kijeshi kutoka pande zilizo kwenye mzozo Libya wamekutana leo mjini Geneva, Uswisi, wakiwa na matumaini ya kupatikana kwa amani ya kudumu itakayosimamiwa na Umoja wa Mataifa katika taifa hilo la kaskazini mwa Afrika lililokumbwa na mzozo kwa muda sasa.



Mkutano huo ni mzunguko wa nne wa mazungumzo yanayohusisha Tume ya Pamoja ya Jeshi chini ya uangalizi wa mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Stephanie Williams ambaye ni afisa wa zamani wa wizara ya ulinzi ya Marekani.

 

Waandalizi wa mkutano huo kutoka Umoja wa Mataifa wanasema mazungumzo hayo yanatarajiwa kudumu hadi Jumamosi na wanatazamia mwafaka upatikane kati ya pande hizo mbili kuhusiana na masuala yote yaliyokuwa na utata kwa ajili ya usitishwaji kamili wa mapigano kote nchini Libya.

Post a Comment

0 Comments