Na: JOSEPHINE MALLANGO MASISI
Matokeo ya utafiti wa Mradi wa Sera ya Kilimo Afrika (APRA), nchini Tanzania yameonyesha kuwa Kilimo Biashara kina manufaa kwa rika zote huku akina mama na vijana wanaonekana kunufaika zaidi kwa kujipatia ajira kupitia mnyororo wa thamani katika kilimo hicho .
Add caption |
Prof. Isinika amesema kilimo biashara ni mkombozi wa kutokomeza umasikini kwa wakulima kwa kuwa kinaboresha tija na ziada ambapo Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imetakiwa kuongeza msukumo katika kutanua wigo wa mazao ya kibiashara ya muda mfupi nchini.
Prof. Isinika ambaye ni Mtafiti Kiongozi wa mradi wa (APRA) amesema mradi ulihusisha zao la Mpunga na Alizeti kwa kuwa ni mazao chanzo cha chakula na uchumi na pia ni mazao ya muda mfupi na walichagua wilayani Kilombero mkoani Morogoro na Ilamba na Mkalama mkoani Singida na kuwafikia Zaidi ya wakulima 500.
Kwa upande wake Mtafiti wa mradi wa Sera za Kilimo Afrika (APRA )Prof. Ntegua Mdoe amesema matokeo ya utafiti wa mradi huo yanaonyesha manufaa kuanzia kwa wakulima wadogo wadogo na jamii zinazozunguka maeneo hayo kwa kujihusisha na kilimo moja kwa moja au katika mnyororo wa thamani
Prof. Mdoe amesema wanaishauri serikali kwa sasa iweke mkazo katika Kilimo Biashara kwa mazao ya muda mfupi huku akisisitiza uwepo wa mifugo katika maeneo ya kilimo kwa wakulima wa kati kwani imeonyesha kuwa na manufaa zaidi kwa matumizi rahisi ya jembe la ng’ombe hasa kwa vijana na akina mama .
Nae Mtafiti Mwandamizi wa masuala ya Kilimo na Jinsia Dkt. Devotha Kilave amesema katika utafiti huo waliangalia mchango wa kilimo biashara katika kumsaidia mwanamke na kwamba uwepo wa uzalishaji mkubwa umeongeza mnyororo wa thamani ikiwepo viwanda vya usindikaji na bidhaa zake zimekuwa zikimpa ajira mwanamke kwa kujialili na kujipatia kipato cha uhakika na kupelekea kujiamini katika kushiriki shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Washiriki Waandishi wa habari kutoka katika vyomba mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi |
Mtafiti wa mradi wa utafiti wa sera ya kilimo afrika(APRA)Prof.Ntengue Mdoe akielezea kuhusu kilimo biashara na manufaa klwa jamii wakiwemo vijana |
0 Comments