Na Gerald
Lwomile
Ilula,
Iringa
Chuo Kikuucha Sokoine cha Kilimo SUA kimesema ili nchi ya Tanzania iendelee katika sekta
ya kilimo juhudi za makusudi zinahitajika katika kuhakikisha wananchi
wanachukua jukumu la kujiletea maendeleo kwa kubadilisha aina ya kilimo na
kufanya kiwe cha kibiashara kwa kutumia mbinu bora za kilimo yaani
kuzipokea na kuzitumia mbinu za wawekezaji wenye nia ya kuikwamua
jamii katika changamoto mbalimbali
Hayo
yamesemwa February 18, 2020 Ilula mkoani Iringa na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda wakati wa ziara ya siku moja
ya kutembelea uwekezaji katika kilimo biashara unaofanywa na “Farm For the Future”
Prof.
Chibunda ambaye katika ziara hiyo aliambatana na viongozi na wataalam
mbalimbali kutoka SUA amesema wananchi katika maeneo mbalimbali nchini kama
watatumia mbinu bora za kilimo na kukubali kuasili mbinu zinazotumiwa na
wawekezaji wakubwa wanaweza kuwa na uzalishaji wenye tija ambao utainua maisha
yao na wataweza kujiletea maendeleo kwani wapo wawekezaji ambao wana nia ya
dhati ya kutaka kusaidia jamii
“Shamba hili linatupa mfano mzuri kwamba watanzania wa kipato cha chini au kipato cha kati ni vizuri tukaweka mazingira mazuri ya kushirikiana na wawekezaji badala ya kugombana nao kwa sababu kuna mengi ya kujifunza kutoka kwao, mfano huyu hapa ameanza kuwafundisha wasichana wadogo ambao wamepata mimba kabla ya kuolewa kulima maharage mabichi yanayosafirishwa kwenda nchi za ulaya…. Kwa hiyo nitoe wito kwa watanzania ni vizuri tunapopata wawekezaji wakweli na wasio matapeli basi tushirikiane nao ili kujiletea maendeleo”
Makamu huyo
wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo ameongeza kuwa SUA itaendelea na
kazi ya kuhakikisha inawafikia wakulima katika maeneo yao kwani hivi sasa
inaangalia uwezekano wa kushirikiana na mwekezaji huyo ili kutumia shamba hilo
katika mafunzo na tafiti kwa wanafunzi wake na matokeo ya tafiti hizo
yatanufaisha wakulima wote nchini kama ambavyo imekuwa ikisisitizwa Rais Mhe.
Dkt John Pombe Magufuli
Akizungumza na SUA Media Meneja wa Mradi huo wa “Farm For the Future” Bw. Osmund Ueland amesema wao pamoja na kuwa na nia ya dhati ya kufanya kilimo biashara lakini pia wamelenga kuhakikisha wanaisaidia jamii ya wana Ilula katika kutambua kuwa kilimo ni moja ya njia kubwa za kujipatia kipato
Amesema kuwa
baada ya wao kupata shamba hilo waligundua kuwa kuna shida katika udongo wa
eneo hilo na kuwa hauna rutuba ya kutosha hivyo kazi kubwa ilikuwa ni
kuhakikisha wanarutubisha udongo huo kwa kutumia njia za kisasa ikiwa ni
matumizi ya mbolea
“Na sasa tunataka pia kutumia njia ya umwagiliaji katika kilimo cha mahindi na macadamia ... Lakini pia ni muhimu kwetu kufanya kilimo cha kibiashara ili kuendelea kuisaidia jamii, tumekuwa na timu ya mafunzo ambapo tumekuwa tukifundisha wakulima wadogo, wanafunzi na jamii kwa ujumla kufahamu kuwa kilimo ni muhimu kwa maisha yetu ya sasa na ya baadae”
Naye meneja
wa shamba hilo Bi. Grace Kimonge amesema pamoja na kuendelea na kilimo biashara
katika eneo hilo lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni
pamoja na hali ya hewa kwani mvua zimekuwa hazina uhakika lakini pia shamba lina
mawe mengi jambo ambalo yanaathiri ufanisi wa kutumia trekta
Shamba laFarm For the Future lina jumla ya ekari 651 ambazo zina mazao mbalimbali ikiwa
ni pamoja na mahindi, alizeti na hivi sasa wanajianda kulima macadamia zao ambalo linadaiwa kuwa na
soko kubwa nje ya nchi.
Zaidi fuatitilia:-
www.ffftanzania.com
http://www.farmforthefuture.net/contact/
http://www.farmforthefuture.net/
VIDEO BOFYA HAPA CHINI
0 Comments