SUAMEDIA

Watafiti kituo cha Utafiti wa mifugo cha TALIRI Tanga wamegundua aina ya maharage yenye kiwango sawa cha protini na soya


Watafiti kituo cha Utafiti wa mifugo cha TALIRI Tanga wamegundua aina ya maharage yenye kiwango sawa cha protini na kile kilicho kwenye soya ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa kirutubisho hicho kwa wazalishaji wa chakula cha mifugo.







Akizungumza na Waandishi wa habari kutoka kanda ya mashariki waliokuwa kwenye mafunzo ya Uandishi wa habari za sayansi yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH, Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt. Zabron Nziku amesema kupatikana kwa aina hiyo ya mbegu ya maharage ni mkombozi kwa wafugaji nchini.

Amesema kwa miaka mingi waqzalishaji wa chakula cha mifugo na wafugaji wamekuwa wakitumia Soya kama chanzo cha Protini kwenye chakula cha wanyama lakini pia imekuwa ikitumiwa na binadamu kwa kiasi kikubwa kama chanzo cha protini lakini sasa kupatikana kwa maharage hayo Meupe kutapunguza kutumia soya kwenye chakula cha mifugo.
“Hya ni mbadala wa soya yana kiwango sawa na soya na kwa wale wenye viwanda vya kutengeneza vyakula vya mifugo mbalimbali lakini tunachokifanya hapa ni kuzalisha kwa wingi na kuwauzia na haya majani yake ni chakula pia ambacho ukichanganya na maharage haya na majani unapata pilau na sio majani tuu” Alisistiza Dkt. Nziku.

Dkt. Nziku amesema pamoja na kuwa na  sifa sawa na Soya Kwenye kiwango cha Protini lakini pia Maharage hayo meupe waliyogundua yana umbo kubwa ikilinganishwa na Soya lakini pia yanaza sana na hivyo kuwezesha wazalishaji wa malisho na chakula cha mifugo kuzalisha kwa wingi katika ekari.

Kwa upande wake Flora Lukindo ambaye ni meneja wa uzalishaji wa teknolojia kituoni hapa amesema kuwa kwa mbegu hizo wafugaji wamezichangamkia sana na kwakuwa zinaweza kuchangwa kwenye chakula cha kuku na nguruwe ambapo kwa mifugo inayocheua wanakula majani lakini kwa ile isiyocheua wanakula mbegu hizo.

Post a Comment

0 Comments