17/09/2019
Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Mlingano kwa kushirikiana na
wadau wengine wa ndani na nje ya Tanzania wameanza utafiti wa kuwezesha zao la
mkonge kutoa bidhaa ya Mvinyo katika zao la mkonge kutokana
na Tanzania kupata nyuzi pekee
ambayo ni sawa na asilimia mbili ya bidhaa zinazotokana na zao hilo.
Mpango huo umebainishwa na Mkuu wa Kituo hicho Dkt. Catherine
Senkoro wakati akizungumza na Waandishi wa habari kutoka kanda ya mashariki na
watafiti wa kanda hiyo waliokuwa kwenye
mafunzo kwa vitendo juu ya uandishi wa habari za sayansi yaliyoandaliwa na Tume
ya Taifa ya Sayansi na teknolojia COSTECH.
Dkt.Senkoro
amesema kwa uasilia wa tafiti wanazofanya kituoni hapo hawajafanya zaidi
utafiti huo lakini wanashirikina na watafiti wa chuo kikuu cha Dar es
salaam,Bodi ya Mkonge na wengine kutoka nchini Marekani katika kuangalia namna
ya kutumia mkonge uliozalishwa kituoni
hapo ili uweze kutumika kuzalisha bidhaa mvinyo.
”Tafiti
zilizofanyika dunia nzima ni lakini sisi cha kufanya ni kuzichukua kuanza kuishauri Serikai ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuona namna ambavyo zitatumika
na nchi iweze kuzalisha bidhaa zingine zaidi ya Nyuzi” Alisema Dkt. Senkoro.
Dkt.
Senkoro amesema kuwa kupitia watafiti wa kituo hicho wameweza kuzalisha aina
bora ya Mbegu ya Mkonge ambayo inatumika sasa duniani kote hasa China pamoja na
teknolojia zingine za kuzuia magonjwa yanayosumbua kilimo hicho.
Kwa
upande wake Mtafiti kiongozi wa zao la Mkonge kituoni hapo Bw. Gerson Mkolongwe
amesema kuwa kwa sasa Tanzania inatumia asilimia
mbili pekee na asilimia 98 inatupwa hivyo watafiti wanaangalia namna gani wanaweza
kusaidia mkonge kutoa bidhaa nyingi.
Aidha
Bw. Mkolongwe amesema mradi utasaidia wakulima wa mkonge katika kuongeza kipato
pale ambapo Mkonge unakifikisha miaka 12 hadi 15 na kutoa lingoti kwani watawauzia
watu wenye viwanda kwaajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali
Bw.
Mkolongwe amesema utafiti unaonesha kuwa Mkonge uliozeeka unakuwa na Sukari
nyingi ambayo hutumika kutengeneza
Kinywaji na kemikali aina ya Ithano hivyo mkulima atapata faida badala ya
kuingia gharama za kuvunja shamba kama ilivyo sasa.
”Ule
mradi ukifanikiwa yale mashina yaliyozeeka hayatupwa tena na wakulima wengi
watajiunga kwenye kilimo cha mkonge kwakuwa faida itakuwa kubwa na itampunguzia
gharama” Alisema Mkolongwe.
Kwa
upande wake Mtafiti mkuu anayeshughulikia masuala ya makala na machapisho
kutoka COSTECH Dkt. Bakari Msangi amesema kuwa tayari kwa sasa kuna mtambo wa
kuzalisha umeme ambao unaingia kwenye greed ya taifa ambao unatokana na mabaki
ya zao la mkonge na hiyo ni dalili njema kuwa wakulima nanchi itanufaika na zao
hilo.
Vilevile
kituo hicho kwa kushirkiana na kituo cha Nyumbu wamebuni mashine inayotembea na
kuchubua Mkonge ili kupata nyuzi hapohapo shambani badala ya utaratibu wa
zamani wa kuvuna na kuusafirisha umbali mrefu kwenda kwenye vituo vya kuchubua
nyuzi.
0 Comments