Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi Duniani ,Mei Mosi yaliyo fanyika kimkoa ndani ya manispaa hiyo katika uwanja wa Jamhuri na kuongeza kuwa mahali pa kazi panapaswa kuwa sehemu yenye upendo na mahusiano mema baina ya mwajiri na mwajiriwa ili kutoa tija inayokusudiwa.
Aidha Mh. Kebwe amewashauri wafanyakazi kujiandaa kustaafu vizuri wakiwa bado katika utumishi kwa kuangalia na kutumia fursa hasa upande wa kilimo kwa kuwa mkoa huo wa morogoro una ardhi nzuri na yakutosha sanjari na hali ya hewa inayofaa kwa kilmo.
Akisoma risala katibu wa chama cha wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano ya simu Bw. Cloud Kobero ameainisha changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ubinafsishaji wa ndani kwa ndani wa viwanda na kushindwa kuwalipa wafanyakazi vizuri na kwa wakati, waajiri kutoa mikataba mifupi mifupi kwa wafanyakazi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Katika hatua nyingine Naibu wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA upande wa Taaluma Prof. Peter Gillah aliyemuwakilisha Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda amewahakikishia wafanyakazi wa taasisi hiyo kuwa menejimenti inatambua changamoto zao na kuahidi kuwa inaongeza kasi katika utatuzi wa changamoto hizo.
Amesema wafanyakazi ni wajibu kufanya kazi kwa bidii na kuepuka majungu kabla ya kudai haki huku akiwapongeza wafanyakazi bora 52 na wafanyakazi hodari 6 ambao wameonekana kufanya vizuri katika utendaji wao wa kazi.
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani MEI MOSI kitaifa yamefanyika mkoani Mbeya huku mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli yakiwa na kauli mbiu isemayo “tanzania ya uchumi wa kati inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora kwa wafanyakazi ni sasa.
0 Comments