Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kimeingia Mkataba wa Makubaliano wa miaka mitano na Chuo Kikuu cha Yeungnam cha Korea Kusini ili kujenga kituo cha kufundishia wakulima vijijini lengo likiwa ni kuendeleza na kuinua kilimo hapa nchini.
Makubaliano hayo yamefanywa May 20 ambapo Makamu Mkuu wa Chuo cha Yeungnam Prof.Changdeog Huh pamoja na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine Cha kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda wamesimamia kutiwa saini Mkataba wa Makubaliano.
Akizungumza mara baada ya makubaliano hayo Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Prof. Raphael Chibunda amesema kuwa makubaliano hayo yatasaidia katika kusambaza teknolojia bora za kilimo vijijini.
Chibunda ameongeza kuwa chuo kitatoa baadhi ya walimu kwenda kusoma shahada ya pili na ya tatu katika Chuo cha Yeungnam cha Korea Kusini ili kuongeza uelewa zaidi katika taaluma zao za kilimo


0 Comments