Mafuriko na mmomonyoko wa udongo umepelekea watu wasiopungua 51 kupoteza maisha katika mkoa wa KwaZulu-Natal, mashariki mwa Afrika Kusini.
Maafa hayo yamesababishwa na mvua kubwa ambazo zinaendelea kunyesha katika mkoa huo tokea siku ya Jumatatu. Mafuriko hayo pia yameharibu maeneo mengi ya makazi pamoja na maelfu ya hekari za ardhi ya kilimo.
Kiwango cha maji kimekuwa kikiongezeka katika mkoa huo na kuwalazimisha baadhi ya wakazi wa viunga vya mji wa Durban ulioko kwenye mkoa huo kuyahama makazi yao.
Ripoti zinasema kuwa miili ya wahanga wa mafuriko hayo inaendelea kuopolewa kutoka kwenye maji ya mafuriko ambayo hadi sasa yamewasababishia wakazi wa maeneo yaliyoathirika maafa na hasara kubwa.
0 Comments