Kaimu Mkurugenzi kitengo cha elimu ya afya kwa umma kutoka Wizara ya Afya Dkt.Amalberga Kasangala, amesema serikali imejipanga kuhakikisha ugonjwa wa Ebola hauingii nchini ambapo jopo la watalaam kutoka wizarani wameshaweka kambi mkoa wa Kagera pamoja na mikoa mingine ya mpakani.
Dkt.Kasangala amebainisha hayo wilayani Bukoba mkoani Kagera, katika kikao cha dharura cha kujadili hatua mbalimbali ambazo zimeshaanza kuchukuliwa na serikali katika kuhakikisha ugonjwa wa Ebola hauingii nchini.
"Kutokana na tatizo ambalo limetokea nchi jirani tumeamua kuhamia hapa Kagera, timu ya watalaam zaidi ya asilimia hamsini kwani mkoa huu na mikoa mingine ya jirani zipo hatarini zaidi na tumekaa kwa pamoja na kuweka mikakati mbalimbali sasa ikiwa ni wiki ya pili kuona ni mikakati gani ya haraka ili kuendelea kuweka mkoa wa Kagera unakuwa salama," amesema Dkt.Ama.
Aidha, Dkt.Ama amesema njia sahihi ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola ni kuzingatia suala la usafi hasa kunawa mikono mara kwa mara hivyo ni muhimu kuweka mikakati ya pamoja kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu Ebola.
0 Comments