SUAMEDIA

WATAFITI NCHINI WAMESHAURIWA KUWASILISHA ANDIKO LOLOTE LA UTAFITI KWANZA KWA WADAU WA UTAFITI KABLA YA KUOMBA KIBALI

Na: Calvin E. Gwabara
Watafiti nchini wameshauriwa kuwasilisha andiko lolote la utafiti kwanza kwa wadau wa utafiti kabla ya kuomba
kibali Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH ili wadau hao waweze kutoa ushauri wao kuhusu utafiti
unaofanywa kwenye sekta yao na hivyo kufanya tafiti kuwa na tija zaidi kwa taifa.


Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu wakati akifungua warsha ya siku
mbili kwa wakuu wa Taasisi za Elimu ya Juu na taasisi za Utafiti na maendeleo nchini kujadili kuhusu maadili,
Taratibu,Sheria na kanuni za kufanya utafiti nchini Kilichoandaliwa na COSTECH kwenye ukumbi wa Taasisi ya
elimu ya kujiendeleza kwenye Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA.
Amesema ili tafiti ziweze kuleta tija zaidia na kuondoa changamoto za kurudia kufanya utafiti kuna kila sababu
ya Watafiti kuwasilisha kwanza mawazo yao kwenye wizara au sekta husika kabla ya kupeleka maombi ya
kufanya utafiti wowote kwenye tume hiyo kwaajili ya kupitiwa na kupata kibali.
Dkt. Nungu amesema kumekuwa na lawama nyingi kwa baadhi ya watafiti kwamba vibali vya kufanya utafiti
vinacheleweshwa na COSTECH kitu ambacho amesema inatokana na wao kuwasiliana na taasisi husika ama
wadau wa utafiti kabla ya kupeleka kwenye kamati maalumu ya kitaifa kupitia na kuwapa ruksa ya kutoa kibali
husika cha utafiti.
’’Mathalani unafanya utafiti kwenye Elimu tunategemea Utafiti wako utakuja kubadilisha ua kuboresha sera
hivyo ni muhimu Wizara ya Elimu iweze kujua kinachofanyika ili nao waweze kutoa neno maana inawezekana
ukafanya utafiti ambao majibu yao wanayo tayari’’ Alisema Dkt. Nungu.
Mkurugenzi huyo Mkuu wa COSTECH ameongeza kuwa eneo lingine ambalo  wadau hao watajadiliana na kutoa
mapendekezo ya pamoja ni namna ambavyo Mtafiti wa ndani aanavyotakiwa kushirki kwenye utafiti wa watu
kutoka nje ya nchi hasa baada ya kugundua kuwa watafiti wa ndani huandikwa tu kwenye makaratasi kukithi
vigezo vya kufanya utafiti lakini hawashiriki na hawafahamu lolote kuhusiana na hatua na utafiti unavyofanyika.
‘’ Taratibu za mtu kufanya utafiti kutoka nje ya nchi zinamtaka mtafiti huyo kuwa na mtafiti kutoka Tanzania
lakini cha ajabu mtafiti wa ndani unapomuuliza kuhusu utafiti unavyoendelea na hatua zilizofikiwa hana majibu
anakuambia anajua mtafiti wan je kitu ambacho sio sawa katika taratibu za vibali vya kufanya tafiti za aina hizo’’
Alifafanua Dkt. Nungu.
Dkt. Nungu amesema haya na mambo mengine memngi ndiyo yaliyotufanya tukusanyike hapa kama wadau uli
tuweze kufahamishana na kupeana ushauri wa namna ya kuboresha namana ya utendaj kazi kwenye eneo la
utafiti ili ziweze kuleta tija nchini.
Kwa upande wake amakamu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Lugano Kusilukaambaye ni mshirki wa warsha hiyo
amesema utafiti unasaidia kutatua changamoto za nchi lakini pia lazima uzingatie vigezo na maadili ya kufanya
taifi ili ulete tija kwa taifa.
Amesema ili Utafiti uingie na kutambuliwa na Taifa lazima upitie COSTECH ambao ndio waratibu wa tafiti zote ili
kuweza kufikia malengo na serikali iweze kuutumia kwa manufaa ya jamii na Taifa badala ya watafiti kuishia kwenye
tasisi zao kabla ya kushirikisha wadau.

Amesema kukutana kwao kwenye warsha hiyo lutasaidia sana wakuu wa taasisi kuweza kuwasaidia watafiti wake
kuweza kutimiza vigenzo na masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa sharia na kanuni za tafiti ili kuwa na Utafiti bora
lakini pia kuwahisha kupata kibali kutoka COSTECH.

Post a Comment

0 Comments