MAFUNZO YA KUENDESHA MITANDAO KUZAA MATUNDA (SUA)
Na: Alfred Lukonge na Tatyana Celestine
Mafunzo
kwa waendesha mitandao kutoka Vitivo, Idara, na Vituo mbalimbali vya
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) yanaendelea tena leo katika
Kampasi ya Mazimbu ikiwa na lengo la kuwaongezea weledi wa kusambaza
taarifa za chuo kwa uraisi kwenye tovuti zao.
Mwezeshaji wa mafunzo Bwana Kundasen Swai akitoa mafunzo jana katika Kampasi ya Mazimbu mkoani Morogoro |
Akitoa
mada mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Kundasen Swai
amebainisha kuwa ili tovuti ipate watembeleaji wengi ni muhimu
kuangalia ubora wa taarifa unazituma ili watu duniani wapate
kuzisoma.
“
Natoa wito kwa kila Idara chuoni SUA kuwa
na tovuti yake na kuhakikisha tovuti hizo zinakuwa na wasifu wa kila
mfanyakazi wa idara hiyo kwani kwa kufanya hivyo nafasi ya chuo
duniani itapanda pamoja na kuongeza wanafunzi pia kukitangaza chuo kwa uwanda mpana”.alisema Swai
Kwa upande wao washiriki waliohudhuia mafunzo hayo walitoa maoni yao ni kwa jinsi gani wamefaidika na mafunzo vilevile mategemeo yao baada ya kumaliza mafunzo yao.
Nae Bi Inosencia Nyanghura alisema kuwa kikubwa ni kupata weledi kila kitu kinaweza kufanyika kwa uhakika.
"masuala ya tovuti nilikuwa naona ni ya watu wenye ujuzi wa Teknolojia ya Mawasiliano pekee lakini baada ya mafunzo haya nimeona vitu ni virahisi na mtu yeyote anaweza kuvifanya" alisema Nyanghura.
Kwa upande wake Bwana Christian Paul ameeleza kuwa imekuwa ni rahisi kwa sasa baada yakupata mafunzo kwani vikwazo ambavyo vilikuwa vinawasumbua haviakuwapo tena.
"matatizo yalikuwa yakitutokea tulilazimika kuwafuata watu wa kituo cha komputa lakini kupitia mafunzo haya sasa nitaweza kutatua matatizo ya kimtandao mimi mwenyewe" alisema Paul.
Semina
hiyo imeandaliwa na Kituo cha Kompyuta chuoni SUA na inategemewa
kufungwa siku ya Jumatano ya tarehe 31/8/2016 huku washiriki
wakitegemewa kutoka na mbinu za kupandisha nafasi ya chuo duniani kwa
njia ya mtandao.
UNYWAJI WA MAZIWA YASIYOCHEMSHWA KUSABABISHA MAGONJWA: PROF. KAZWALA
Rebeka
Nyaulingo
Imeelezwa
kuwa unywaji wa maziwa ambayo hayajachemshwa kuna uwezekano mkubwa wa kupata
vimelea vya magonjwa mbalimbali kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.
Akizungumza
na Suamedia ofisini kwake Profesa Rudovick Kazwala amefafanua kuwa maziwa
mabichi yanavimelea mbalimbali vya wadudu ikiwa ni Tb pamoja na bluselasi
ambapo humfanya binadamu kupata homa za mara kwa mara na wakati mwingine
ugonjwa na kushindwa kuendesha maisha ya
kila siku.
Aidha
Prof Kazwala amesema kuwa magonjwa haya ambayo yanatokana na wanyama mara
nyingi yanapoingia kwenye mwili wa mwanadamu humfanya mtu kupata homa za mara
kwa mara na kukosa nguvu kazi ya uzalishaji mali na kushuka kiuchumi kwa taifa.
Wakati
huo huo Prof Kazwala amefafanua kuwa vimelea hawa wa Bluselasi na Tb
wamefanikiwa kuwashambulia zaidi jamii ya wafugaji katika maeneo ya kilosa, Mvomero,
Manyara, Kiteto, pamoja na Arusha kutokana na kutochemsha maziwa kwa ufasaha.
Hata
hivyo watu wa jamii zote wanatakiwa kuwa makini na afya zao kwa kujali kuchemsha
maziwa kwa umakini zaidi kwa lengo la kuondokana na magonjwa yanayoambukizwa
kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.
NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
ZATEGEMEA MALIGHAFI KUTOKA NJE
Rebeka
Nyaulingo
Imeelezwa kuwa nchiza Afrika
Mashariki zimekuwa na uzalishaji mdogo wa malighafi nahivyo zimejikuta
zikitegemea nchi za bara la Ulaya pamoja na China jambo linalopelekea kudumuza
uchumi wake.
PICHA NA MTANDAO |
Akizungumza na Sumedia na
wadau mbalimbali wanaojihusisha na uchumi
Profesa Joseph Hella amebainisha kuwa halihiyoinatokananauhafifu wa miundombinu
yauzalishaji wa bidhaa na hasa viwanda.
Aidha Profesa Hela amebainisha kuwa kutokana na
uhafifu wa miundombinu ya uzalishaji wa bidhaa ndio unaosababisha nchiza
Rwanda, Kenya, Uganda, Tanzania na
Uganda kuwa ni watu wa kupokea zaidi
kuliko kutoa na hilo amesema kuwa katika
ushindani wa kukua kwa masoko China ipo juu kuliko nchi za bara la Ulaya .
Profesa Hella kwa sasa
anafanya utafiti wa zao la pamba isiyotumia dawa wala mbolea katika Wilaya ya
Meatu ,Maswa, Saranda Dodoma ,Mbeya, Mtwara pamoja na Shinyanga utafiti
unaoweze kuwanufaisha wakulima.
WAKAZI WA MOROGORO WATOA MAONI YAO KUHUSU MAZOEZI YA POLISI
Baadhi
ya Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wametoa maoni yao kuhusu kitendo cha jeshi la
polisi hapa nchini kuwa katika mazoezi
makali ya kijeshi yanayoendelea nchi nzima.
PICHA NA MTANDAO |
Wakizungumza
na SUAMEDIA Bw. Sadiki Ramadhani na Bw. Godfrey Mlay wakazi wa Tumbaku Mjini
Morogoro wamebainisha kuwa mazoezi yanayofanywa na polisi yanawatia hofu ya
kutokea mapambano kati ya polisi na vyama pinzani yaani UKAWA.
Wamesema
kuwa mazoezi haya ya kijeshi yanayoendelea yanawapa hofu na kudhani kuwa kukawa
na mapambano makali baina ya pande hizo mbili siku ya tarehe moja mwezi wa tisa
kama yalivyoandaliwa na kutangazwa Vyama vya upinzani nchi nzima.
Kwa
upande wake Bi. Tatu Shomari mkazi wa Mafiga Mjini Morogoro amesema kuwa watu
wasijenge hofu kwani mazoezi yanayoendelea inasemekana nikatika kuimarisha
jeshi lapolisi na sio maandalizi ya kupambana na kitu chochote za kisiasa.
WAKULIMA WAMETAKIWA KUTUMIA MBEGU ZA MAHINDI ZINAZOSTAHIMILI UKAME
Na.Suzane Cheddy.
Wakulima
nchini wametakiwa kutumia mbegu bora za mahindi
zilizofanyiwa utafiti na mbazo zimewekewa uwezo wa kukabiliana na
changamoto ya ukame ili kumhakikishia mkulima kupata mazao bora badala ya
kutumia mbegu za asili mbazo hazina uwezo huo na kusababisha mkulima kupata
hasara kila mwaka.
Wito huo
umetolewa na Mtafiti mkuu kiongozi kutoka
tume ya taifa ya sayansi na teknologia ( COSTECH) Dr.Nicholas Nyange wakati akiongea na SUA
MEDIA juu ya mafanikio yaliyopatikana katika kuzalisha mahindi chotara
yanayostahimili ukame kupitia mradi wa WEMA.
Amesema ukame ni tatizo kubwa linalokumba
maeneo mbalimbali ya Tanzania na nchi jirani ndio maana Mradi huo unashirikisha
pia watafiti wan chi nyngine ambazo ni Uganda,Kenya,Msumbiji ,afrika ya kusini
na washirika wa kimataifa katika kutafuta teknolojia itakayoweza kumsaidia
mkulima wa mahindi kulima kilimo chenye tija na kumuondoa kwenye hasara kila
mwaka.
Dr.
Nyange amesema Utafiti huu ulianza mwaka 2009 kwa lengo la kutafuta mbegu
chotara ambazo zinaweza kustahimili ukame na mpaka sasa mradi huo imefanikiwa kupata aina sita ya mbegu
zinazostahimili ukame huku aina nne kati
ya hizo zimeidhinishwa na waziri wa kilimo,uvuvi na mifugo kwa ajili
ya kupelekwa sokoni.
Mtafiti
huyo kiongozi toka COSTECH
ameongeza kuwa utafiti umeweza
kuleta mafanikio makubwa kwa wakulima walioanza kutumia mbegu hizo za
mahindi zinazostahimili ukame.
SUAMEDIA KUPONGEZWA KWA KAZI WANAYOFANYA MKOANI MOROGORO
Na: Ayub Mwigune
Wadau
mbalimbali wa Manispaa ya Morogoro wamesifu kazi nzuri inayofanywa na SUAMEDIA
katika kutoa elimu mbalimbali hususani kilimo, kuburudisha na kusaidia jamii
kupitia vyombo vyake vya habari.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti kwa nyakati na
mwandishi wa habari hii wamesema wamekuwa wakifuatilia habari zinazo andikwa
kwenye blog ya SUAMEDIA zimewafanya wawe mstari wa mbele katika kuata habari
zinazoendana na wakati.
Christian
Jawadu ambaye ni Mkazi wa Mafiga amesema yeye ni mfuatiliaji sana wa habari
zinazo andikwa na SUAMEDIA na amewapongeza wandishi wa habari wa kituo hicho
kwa kuandika habari ambazo zimekuwa za kweli na uhakika pia amewaomba waweze
kufungua kurasa za mitandao ya jamii kama facebook na twiter iliwa waweze
kufikia jamii kubwa ya vijana wanaotumia
kwa wingi mitandao hiyo.
Naye
Ramadhan Daraja amewasifu SUAFM kwa nyimbo mbalimbali ambazo zimekuwa
zikichezwa na kituo hicho kwani zimekuwa zikilenga makundi mbalimbali ambayo
yapo katika jamii kama vile vijana, wazee pamoja na waumini wa dini hivyo kufanya
jamii kuburudika na kuelimika kupitia kituo hicho.
Naye
mwanamziki wa bongofleva Hanset Wyclef
maarufu kama Hansreal amesema uwepo wa SUAFM utasaidia kukuza na kuinua vipaji
vya wasanii wachanga nchini Tanzania
kwani imekuwa ni vigumu nyimbo zao kuchezwa radio nyingine lakini SUAFM
imekuwa haina ubaguzi huo hivyo imetoa wito waendelee kufanya vizuri ili kukuza muziki wa Tanzania
hususani kusaidia wasanii wachanga waweze kupata nafasi ya kusikika nyimbo zao.
WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUSHUGHULIKIA MTO KIKUNDI MOROGORO
Na: Lucy Mndeme
Wananchi wanaoishi kando kando ya mto Kikundi
unaopita katikati ya Manispaa ya Morogoro, wameiomba serikali ya mkoa huo
kutafuta uwezekano wa kuuchepusha, ili usipite katikati ya mji.
Baadhi ya wananchi hao wameiambia SUAMEDIA kuwa mto
huo ambao wakati wa kiangazi hukauka, umesababisha kuwepo kwa madaraja mengi
katikati ya mji.
Mmoja wa wananchi hao Juma Mohamed Mkambi amesema
mto Kikundi una madaraja zaidi ya matano kutokana na kupita katikati ya
manispaa ya Morogoro.
Amesema kutokana na gharama kubwa za kuhudumia
madaraja hayo, mto huo ungeweza kuchepushwa na kupita eneo la Chuo cha Mifugo
LITI na kuingia mto Morogoro, hivyo kuondoa usumbufu wa kuhudumia madaraja
ambayo hayana tija kwa wananchi.
Mkambi amesema mto huo ambao maji yake si safi na
salama, hautoi huduma yoyote kwa wananchi wanaoishi kandokando ya mto huo,
zaidi ya kugeuzwa dampo la taka ngumu na maji taka kufuatia baadhi ya wakazi
waliojenga kando ya mto huo kuelekeza maji ya vyooni kwenye mto huo.
Naye mwananchi mwingine
aliyeomba jina lake kuhifadhiwa aliiomba idara ya afya Manispaa ya Morogoro
kuwazuia wakulima wadogo wa mboga za majani kutumia maji hayo kunyweshea
bustani zao, kutokana na maji hayo kuwa na kila aina ya uchafu, hivyo
kuhatarisha maisha ya watumiaji wa mboga hizo.
KILO 370 ZA NYAMA POLI ZAKAMATWA KIJIJI CHA BWAKILA MOROGORO VIJIJINI
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro
linamshikilia mtu mmoja baada ya kumkuta na nyamapori kilo 370 katika kijiji
cha Bonye Tarafa ya Bwakila Wilaya ya
Morogoro vijijini.
Tukio hili limetokea mnamo tarehe 19 augost mwaka huu majira ya
saa3:30 asubuhi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda
wa Polisi Mkoani Morogoro Ulrich Matei amesema tukio hilo limetokea Jumamosi
Agosti 19 saa 3.3 asubuhi na kuwa
mtuhumiwa huyo ambae anajulikana kwa jina la Koba Nasibu alikutwa na
nyama ya Pundamilia Kg 260, Nyumbu kg 50, Swala kg 40 pamoja na nyama ya Ngiri
kg 20.
Aidha kamanda Matei amesema kuwa mtuhumiwa
huyo amekamatwa na viungo mbalimbali vya wanyamapori hao ikiwa ni mikia miwili
ya pundamilia, pembe mbili za nyumbu, pamoja na pembe mbili za swala.
Hata hivyo kamanda Matei amesema thamani ya
nyama na viungo vya wanyamaori hao bado haijafahamika.
WAFUGAJI WAMPIGA HADI KUFA MKULIMA WILAYANI KILOSA
Na:Ashura Janati
Kijana mmoja Mkazi wa Kijiji cha Tindiga Wilaya
ya Kilosa amefariki dunia baada ya kupigwa na wafugaji wa kimasai waliokuwa
wakilisha mifugo yao shambani kwake.
Diwani wa kata ya Tindiga Mhe. Yahya
Mbaruku Mbachi amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kumtaja kijana
aliyeuawa kuwa ni Ali Mbaruku Makakala na tukio hilo limetokea tarehe 16
Agosti majira ya mchana.
Mhe. Mbachi amesema taarifa ilifika
kijijini kuwa wafugaji hao wa kimasai walikuwa wakilisha mifugo yao katika
mashamba ya wanakijiji, na marehemu Makakala na vijana wengine ambao ni polisi
jamii wa kijiji hicho walikwenda kuhakiki ukweli wa taarifa hizo.
Amesema walipokaribia eneo walipokuwa
wakilisha mifugo hiyo marehemu alibaini kuwa ng’ombe hao wako shambani kwake
ndipo alipokimbia kuelekea huko na kuwaacha nyumba vijana wenzie lakini
akashambuliwa na wafugaji hao kusabababisha kifo chake papohapo na wafugaji hao
wakatokomea na ng’ombe zao.
Kufuatia hali hiyo wananchi wa kijiji cha
Tindiga waligoma kumzika marehemu wao hadi mkuu wa wilaya ya Kilosa afike eneo
la tukio na imeelezwa baadaye mkuu huyo wa wilaya ya Kilosa alifika na kuagiza
kuheshimiwa kwa mipaka kati ya Tindiga kwa wakulima na Mkata ndio kwa wafugali
eneo linaloitwa Samunge.
Juhudi za jeshi la polisi zinaendelea
kuwasaka watuhumiwa hao ni mkondo wa sheria ufuate.
WANANCHI
WA LUKOBE KUKAIDI AGIZO LA MKURUGENZI WA MANISPAA
Na: Mazoea Iddy
Wananchi wa Kata ya Lukobe
Manispaa ya Morogoro wameendelea kufanya shughuli zinazodaiwa kusababisha
uharibufu wa mazingira katika kingo za mto Ngerengere licha ya kupewa notisi
Akizungumza na SUAMEDIA Afisa
Mtendaji Kata ya Lukobe Bw. Selemani Mjata amesema kuwa zuio lililotowa mnamo
25/11/2015 kukataza kufanya shughuli yoyote ambayo itaweza kuharibu kingo za
mto huo lakini wananchi hao bado wamekaidi agizo hilo.
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti
wa Mtaa wa Tuelewane Bw. Ally Mohamedi Gwandu ameeleza kuwa wananchi hao bado
wanaendelea kufanya shughuli za kilimo cha mboga mboga na ufyatuaji wa
matofali.
Ameongeza kuwa Viongozi wa Mtaa wamejipanga
kwa dhati ikiwezekana kutumia vyombo vya dola ili kuwaondoa katika maeneo hayo
hatarishi kwa mazingira
Aidha wananchi wa Kata wameiomba serikali
kuwatafutia sehemu halali ya kufanyia shughuli hizo ili kuhepusha uharibifu wa
mazingira kwani wanalazimika kufanyia eneo hilo kwa kujiingizia kipato.
TEMBO AVAMIA KIJIJINI NA KUUA MTU MMOJA
Na: Mazoea Iddy
Mnyama aina ya Tembo amevamia
katika Kijiji cha Kilangalimkata Tarafa ya Kimamba Wilaya ya Kilosa Mkoa wa
Morogoro na kusababisha mauaji ya Samson Jakob mwenye umri wa miaka 35 ambaye
ni Mkazi wa Kijiji hicho.
Akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Leonce Rwegasira alisema kuwa
tukio hilo limetokea mnamo tarehe 12/08/2016 majira ya saa saba usiku.
Taarifa zinasema kuwa, Tembo huyo alivamia kibanda shambani kwa marehemu akiwa amelala na kukivunja ambapo
marehemu alifariki dunia mara baada ya kukanyagwa na Tembo sehemu mbalimbali za
mwili wake.
Aidha Jeshi la Polisi limesema
kuwa linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.
MWANAMKE AKUTWA AMEKUFA HOTELINI KILOSA MKOANI MOROGORO
Na: Ashura Janati
Mwanamke
mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 38 anayejulikana kwa jina la Mwajabu Kilosound Mkazi wa Kilosa Mjini mkoani Morogoro
amekutwa amefariki dunia akiwa hotelini mjini Kilosa.
Tukio
hilo liligunduliwa siku ya Jumapili agosti 14 kunako saa 5 asubuhi baada ya mhudumu wa hoteli hiyo kumkuta marehemu akiwa katika chumba
alicholala na kutoa taarifa kwa mmiliki wa hoteli hiyo.
Akizungumzia
kifo hicho Kaimu Kamanda wa Polisi wa Wilaya
ya Kilosa aliyefika katika eneo la tukio Eusebio Nyalifa amesema ukaguzi wa
awali unaonyesha kuwa marehemu amefariki dunia akiwa hana jeraha lolote mwilini mwake.
Kwa
mujibu wa watu waliokuwa karibu na marehemu Mwajabu waliielezea SUAMEDIA kuwa
katika siku za karibuni alikuwa na
mahusiano na mwanaume ambaye alikuwa mgeni katika eneo hilo na baada ya tukio
hilo mwanaume huyo alitoweka na hadi sasa haijulikani alipoelekea.
Nao
watoto wa marehemu wamesema kuwa
mwanaume huyo alikwenda asubuhi katika duka lao la vinywaji na kuwaambia yeye na mama yao wanasafiri
hivyo wampe fedha za mauzo ya dukani na kuongeza kuwa waendelee na ratiba zao
za kila siku.
Jeshi
la polisi likishirikiana na wananchi linaendelea kumtafuta kijana huyo aliyekuwa na marehemu katika hoteli hiyo.
BW. MRISHO GAMBO KUWA MKUU WA MKOA WA ARUSHA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha,Mrisho Gambo aliyeteuliwa na Rais,kuapishwa kesho ijumaa Ikulu jijini Dar |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix
Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa
Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Gambo
alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016)
saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
UNYANYASAJI WA KIJINSIA WALETA ATHARI ZA KISAIKOLOJIA SUA
Madhara ya Unyanyasaji wa Kijinsia yameonekana
kuleta athari kubwa kisaikolojia, kimwili na kupelekea kupungua kwa tija uande
wa wafanyakazi na kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Hayo yamesemwa na Dokta Sotco Komba alipokuwa
akitoa mrejesho kuhusu utafiti wa Unyanyasaji wa Kijinsia kwa wafanyakazi na
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo katika hafla ya uwasilishaji matokeo ya utafiti
iliyofanyika chuoni hapo.
Dkt Komba amesema malengo ya utafiti huo ni
kuwezesha kupatikana kwa uelewa wa kina kuhusu hali na ukubwa wa tatizo la
Unyanyasaji wa Kijinsia chuoni SUA na
kutoa mapendekezo ya namna bora ya kikabiliana na tatizo hilo.
Kadhalika Dkt Komba amesema baadhi ya mambo yanayopelekea kuwepo
kwa unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na tabia binafsi za watu, mavazi yanayoshawishi, kiwango
kidogo cha mikopo na kuchelewa kwa fedha ya chakula
kutoka bodi ya mikopo, na uwepo wa wafanyakazi wengi wasiofahamu haki na
kanuni za kazi zilivyo.
Pia Dkt Komba amefafanua zaidi kuwa utafiti huo
umebaini madhara ya kisaikolojia
yameonekana kuwa na asilimi 94.4 , madhara ya kimwili ni asilimia
5.6 huku watekelezaji wa vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia ni wanafunzi wa
kike asilimia ambao wanavaa nguo zisizo na staha kwa asilimia 34.3 wanafunzi wa kiume kwa asilimia 31.5 na wanataaluma wa
kiume kwa asilimia 15.4 wakati wa mafunzo kwa vitendo.
Upande wa wafanyakazi waliohudhuria katika hafla
hiyo Bw.Erasto Mnyatu amewaomba watafiti hao kuweka mapendekezo kwa Chuo kuunda
chombo huru chenye uwazi cha kusimamia
matatizo ya kesi za unyanyasaji wa kijinsia ndani ya
taasisi.
Utafiti wa
unyanyasaji wa kijinsia kwa wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo umefanywa na Profesa
Aida Isinika na Dkt Sotco Komba chini ya
kamati ya Chuo inayojihusisha na
utekelezaji wa sera ya jinsia (GPIC) na
kitengo cha Jinsia katika mradi wa iAGRI lengo likiwa ni kujua hali ya tatizo
hilo hapa SUA.
MTU MMOJA MKOANI MOROGORO ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA ULAWITI
Na: Fadhila Kizigo
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro
linamshikiria mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Alhaj Hussen Doto [27] mkazi
wa sabasaba kwa tuhuma za kuwalawiti watoto wawili majina yanahifadhiwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro
ACP Leonce Rwegasira amesema kuwa mnamo Agosti 13 mwaka huu majira ya saa tano
usiku maeneo ya Uwanja wa Taifa manispaa ya Morogoro, mama wa mtoto mmojawapo
aligundua kuwa mtoto wake wa miaka mitatu amelawitiwa.
Kamanda Rwegasira amesema mama wa
mtoto huyo aligundua baada ya mtoto kulalamika kuwa na maumivu makali sehemu yake
ya siri yeye na mtoto mwenzie jina linahifadhiwa mwenye umri wa miaka [5] wote
ni majirani na wakazi wa uwanja wa taifa.
Ameeleza aliwagundua kuwa
wamefanyiwa kitendo hicho na baada ya
kuwadadisi watoto hao walimtaja mtuhumiwa aliyewatendea kitendo hicho ambaye ni
Alhaji Hussen Dotto.
Kamanda Rwegasira amesema kuwa
watoto wanaendelea na matibabu katika hospital ya rufaa mkoa wa Morogoro pia
mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi
kukamilika.
VYETI BANDIA ZAIDI YA 1000 VYANASWA
Sehemu ya vyeti bandia zaidi ya 1000
kwa ajili ya Taaluma ya uuguzi ufundi mbalimbali ambavyo vimekamatwa na
polisi mkoani Kigoma kwa kushirikiana na maafisa wa Baraza la Wafamasia vyeti
ambavyo vilikuwa tayari kugawanywa kwa ajili ya matumizi ya kuwapatia watu ili
vitumike kutafutia ajira.
(Picha na Fadhili Abdallah)
PONGEZI KWA KITUO CHA RADIO SUAFM
Na.Adam Ramadhan
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva na Hip-hop) wametoa shukrani zao za dhati kwa kituo cha redio cha
SUAFM kinachorusha matangazo yake kwa majaribio kutoka mkoani Morogoro kwa kusapoti
na kupiga Muziki wao.
Wakizungumza na SUAMEDIA baadhi
ya wasanii waliofanya mahojiano
mafupi wametoa shukrani zao kwa
Uongozi na wafanyakazi wa kituo hicho
kwa kuzipiga bure nyimbo zao ambazo wamekuwa wakizileta kituoni hapo.
Emanuel Kasolela(27) aka Pacha B ni msanii wa Bongo
Fleva amesema kuwa licha ya nyimbo zake
kupigwa kwenye kituo cha SUAFM amekuwa akikutana na changamoto kubwa ya
kipato na sapoti ya nyimbo zake kupigwa kwenye redio.
Kassimu Bochu aka Bochu amesema kwa chipukizi wanaoanza muziki inatakiwa wapewe kipaumbele ili waweze
kufikia malengo na hivyo anaipongeza SUAFM kwa kuzipiga nyimbo zote za
wasanii wa Morogoro.
SUAFM ni redio inayorusha
matangazo yake kwa majaribio kutoka mkoani Morogoro ikiwa katika masafa ya
101.1 huku ikishika takribani mikoa 10 nchini Tanzania.
0 Comments