SUAMEDIA

WATANZANIA WATUMIE MFUMO WA AFYA DATA KUTOA TAARIFA KUHUSU DALILI ZA MAGONJWA

Na:Farida Mkongwe
Wakazi wa Mkoa wa Morogoro na watanzania kwa ujumla wameshauri
wa kuutumia mfumo wa Afyadata ambao unatoa taarifa za dalili za
magonjwa mbalimbali kwa haraka na hivyo kuweza kupata tiba
itakayookoa maisha yao.


Ushauri huo umetolewa na Afisa Mtawala wa Mradi wa DODRES- SAC
IDS uliopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Robert Maduka wakati akizungumza na SUAMEDIA kuhusu umuhimu wa mfumo wa Afyadata kwa maisha ya binadamu.
Maduka amesema mfumo huo wa Afyadata unapatikana kwenye simu
za Android na kwamba anachotakiwa kufanya mtumiaji ni kupakua
programu ya Afyadata na hapo ataweza kupata fomu atakayojaza
namna anavyojisikia na baadae atapata mrejesho wa dalili za ugonjwa
alionao.
Akizungumzia changamoto zilizopo katika matumizi ya Afyadata
amesema watu wengi na hasa wanaoishi vijijini bado hawajawa na
uelewa na mwamko wa kutosha kuhusu mfumo huo  na wao
wanaendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali yakiwemo
maeneo ya vijijini.
“Matumizi ya Afyadata siyo magumu kabisa cha msingi ni watu kuwa
tayari kutumia teknolojia mbalimbali ambazo zinajitokeza kwa sababu
hakuna namna ya kuepukana na teknolojia za kisasa katika karne hii
ya sayansi na teknolojia”, alisema Afisa huyo.



Post a Comment

0 Comments